Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, July 22, 2013

PICHA::YANGA YATOKA SARE NA URA YA UGANDA


Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kuzawazisha dhidhi ya URA ya Uganda, lililofungwa na Jerson Tegete katika dakika ya 90 ya mchezo na kufanya matokeo kuwa 2-2. Mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki umefanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. URA jana ilicheza na Simba na kuifunga 2-1.


Mshambuliaji wa URA ya Uganda, Lutimba Yayo akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa Yanga, Ibrahim Job na Rajabu Zahir katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Beki wa URA ya Uganda, Lutimba Yayo akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Yanga, Jerson Tegete katika mchezo wa kimataiafa wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2. 


Wachezaji wa URA wakishangilia bao la pili la timu hiyo.


PICHA ZOTE KWA HISANI YA HABARI MSETO BLOG

No comments:

Post a Comment