Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, July 22, 2013

IFAHAMU VYEMA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI VISABABISHI NA KINGA ZAKE


UTAFITI mpya wa kitabibu umebaini kuwa saratani ya shingo ya kizazi, inasababishwa pamoja na mambo mengine na ngono kama ilivyo kwa ugonjwa wa Ukimwi, madaktari bingwa wa magonjwa ya maradhi hayo wamesema. Madaktari bingwa wa uchunguzi wa magonjwa katika Kitengo cha
Patholojia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, na Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Madaktari hao wametaja mambo mengine yanayoweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazi kuwa ni kujiingiza kwenye
mapenzi katika umri mdogo, kuolewa mara nyingi, kuwa na wapenzi wengi, kusafisha
sehemu za siri kwa bidhaa zenye kemikali na kuzaa mara nyingi.

No comments:

Post a Comment