Rais
wa Marekani, Mhe. Barack Obama Amewasili nchini leo tarehe
01 Julai, 2013 mchana kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.Katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam,
Mhe. Rais Obama ambaye amefuatana na Mkewe Mama Michelle amepokelewa na
Mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya
Mrisho Kikwete.Baada
ya mapokezi, Mhe. Rais Obama atakwenda Ikulu kwa mazungumzo rasmi na
Rais Mhe. Kikwete. Aidha, atafanya mkutano na Wafanyabiashara na
kuhudhuria Dhifa ya Kitaifa.Tarehe
2 Julai 2013, Mhe. Rais Obama atatembelea Mitambo ya kufua Umeme ya
Symbion iliyopo Ubungo, Dar es Salaam na kuzindua rasmi Mpango Maalum wa
Maendeleo ya Nishati Barani Afrika ulioanzishwa na
Marekani (Power Africa Initiative).Mpango huo utaanza na nchi saba ambazo ni: – Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia, Ghana, Nigeria na Sudan Kusini.Mhe. Rais Obama anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 02 Julai 2013.IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM

Monday, July 1, 2013
-On Monday afternoon, President Obama takes part in a formal arrival ceremony in Dar es Salaam, Tanzania.
-President Obama participates in a bilateral meeting and joint press conference with President Jakaya Kikwete of Tanzania.
-In the evening, President Obama participates in a CEO roundtable and business leaders forum.
-President Obama and President Jakaya Kikwete of Tanzania participate in an official dinner.
Tuesday, July 2, 2013
Tuesday, July 2, 2013
-On Tuesday morning, President Obama takes place in a Consulate meet and greet.
-President Obama visits the Ubungo Power Plant.
alipowasili
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na ndege yake
Air Force One, Rais wa Maekani, Barack Obama amezindua barabara mpya
upande wa Mashariki wa lango la kuingia Ikulu ambayo inatarajiwa kuitwa
Barack Obama.Baada
ya shughuli hiyo atazungumza kwa nyakati tofauti na wafanyabiashara wa
nchi za Afrika na Marekani kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Dar es
Salaam. Amepanga pia kuzungumza na maofisa wa Ubalozi wa Marekani
nchini.Baadaye atahudhuria dhifa ya taifa usiku ambayo imeandaliwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.Kesho
ataweka shada la maua sehemu ulipokuwa Ubalozi wa Marekani ikiwa ni
kumbukumbu ya watu waliouawa katika shambulizi la kigaidi la bomu mwaka
1998, Dar es Salaam. Pia atatembelea mitambo ya kufua umeme ya kampuni
ya Symbion iliyoko Ubungo.
Rais Obama atatoa hotuba kuzungumzia mikakati ya Marekani ya kusaidia Afrika kuzalisha nishati ya umeme.
Michelle atakuwa na ratiba yake ambapo atapata staftahi na mwenyeji wake, Salma Kikwete katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), Dar es Salaam.
Pia atatembelea sehemu ulikokuwa ubalozi wa Marekani na kisha atashuhudia onesho la utamaduni la kikundi cha Baba wa Watoto, ambacho kinajumuisha watoto wa mitaani wenye umri wa kuanzia miaka mitano hadi 18 kwenye Makumbusho ya Taifa.
Jumanne, Michelle atahudhuria mkutano na wake wa marais wa nchi za Afrika ambao pia utahudhuriwa na mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush, Laura.
Julai 2, Rais Obama atatembelea mitambo ya kufua umeme ya Symbion Ubungo saa 4 asubuhi na kisha msafara wake utapita Nelson Mandela, Tazara hadi uwanja wa ndege na kuondoka saa 5.20 asubuhi.
Obama ametangaza mpango wa kuwajengea uwezo viongozi vijana wa Afrika kwa kuwapa mafunzo ya uongozi katika vyuo vikuu vya Marekani hasa katika masuala ya utawala, biashara na uongozi.
Katika hotuba yake katika Chuo Kikuu cha Johannesburg juzi jioni, alisema hatma ya Afrika iko mikononi mwa vijana; hivyo ni lazima wawezeshwe ili kuliongoza vizuri bara hili.
Alisema mafunzo hayo yatatolewa chini ya mpango wa ufadhili wa Marekani kwa viongozi vijana ambao utawajengea uwezo wa kuendesha huduma za kiserikali ikiwa ni pamoja na biashara na kuhudumia jamii yao.
Kuanzia mwaka ujao Marekani itatoa mafunzo kwa vijana 500 ambayo yatakuwa ya wiki sita ambapo idadi hiyo itaongezeka hadi vijana 1,000 kila mwaka.
Watakaofadika ni vijana wa kati ya umri wa miaka 25 hadi 35 ambao wamekuwa wakijihusisha na uongozi ndani ya Serikali, sekta binafsi na asasi za kiraia. Alisema washiriki hao ni lazima waoneshe dhamira yao katika kuitumikia jamii.
Obama alisema Afrika ina mwonekano mzuri kwa siku zijazo na kuwataka vijana wa Afrika kuhakikisha wanatumia uwezo wao katika kutumikia bara lao.
Mpango wa kuendeleza vijana wa Afrika ujulikanao kama YALI ulizinduliwa mwaka 2010 na Rais Obama ikiwa ni sehemu ya kusaidia maendeleo, kuhamasisha ujasiriamali na kujenga uwezo wa Afrika kuwa na viongozi bora wa kizazi kijacho.

No comments:
Post a Comment