WAJASIRIAMALI
nchini pamoja na vijana wameshauriwa kutumia fursa mbalimbali za
maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali katika kutangaza Biashara zao
pamoja na kutengeneza fursa ya kupata masoko ya kudumu ya bidhaa
wanazozalisha kwa lengo la kujiajiri, kujiongezea kipato na kukua
kibiashara
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Kampuni ya
African Centre for Business Consultancy (ACBC Consultancy) Bw.Rashid
Adam wakati akizungumzia maonyesho yajulikanayo kama “Free Marketing
Zone Exhibition” yatakayofanyika katika Viwanja vya Nyerere (Nyerere
Square) Mkoani Dodoma kuanzia tarehe 31 Agosti hadi 6 Septemba 2013.
Bw.
Adam amesema kuwa maonyesho ya Free Marketing Zone yamelenga zaidi
kuwatafutia masoko ya kudumu wajasiriliamali mbalimbali pamoja na
makampuni yatakayoshiriki kwa lengo la kukuza biashara zao pamoja na
kuwakutanisha wajasiriamali na makampuni tofauti ambapo watabadilishana
uzoefu na fursa mbalimbali za kibiashara
Aidha
Mkurugenzi huyo amesema kuwa wajasiriamali wengi wanatengeneza bidhaa
nzuri lakini wanakosa masoko ya uhakika kutokana na bidhaa zao
kutojulikana kwa walaji .
“Wajasiriamali
wengi wanatengeneza bidhaa nzuri ,nyingine ukiziona huwezi amini kama
zinatengenezwa nchini lakini wanashindwa kuuza bidhaa hizo kutokana na
kukosa wateja na masoko kwa kutojulikana kwa bidhaa hizo .na
wateja.”alisema Bw.Adam
Bw.Adam
amewakaribisha wananchi na wajasiriamali kushiriki katika Maonyesho
hayo ili wapate fursa ya kukutana na watu tofauti wenye ujuzi na mawazo
tofauti yatakayosaidia kuboresha huduma na bidhaa wanazozalisha,vilevile
kuwawezesha wateja kuwajua na kupata bidhaa hizo moja kwa moja.
Mkurugenzi
huyo ameeleza kuwa wajasiriamali watakaoshiriki watapewa vyeti vya
ushiriki pamoja na nafasi ya kutangaza biashara zao katika jarida
litakalokuwa na anuani za washiriki wote, zikionesha biashara zao na
sehemu wanapopatikana ili wateja waweze kuwafiki kiurahisi baada ya
maonyesho hayo pamoja na kuwatangaza zaidi kibiashara.
Bw.
Adam amewakaribisha wajasiriamali wote wanaopenda kushiriki maonyesho
hayo ya Free Marketing Zone Exhibition ili waweze kuwafikia kiurahisi
wateja wao na kutanua wigo wa masoko kwa bidhaa zao, huduma zao na
Biashara zao.
No comments:
Post a Comment