Gari la Wakili Erasto baada ya kugonga likiwa Kituo cha Polisi Wazo Hill.
Na Makongoro Oging'
ASKARI
polisi wa usalama barabarani wa Kituo cha Oysterbay jijini Dar es
Salaam, Amani Leon amenusurika kuuawa kwa risasi na Wakili Erasto
Lugenge wakati akipima ajali ya magari.
Tukio
hilo lilitokea Julai 13, mwaka huu, saa 6.30 usiku Boko CCM, wilayani
Kinondoni ambapo askari huyo alimtaka Lugenge wafike kituoni kutoa
maelezo.
Chanzo
chetu cha habari kimeeleza kwamba Leon alipata taarifa kwamba Leon
alipata taarifa kwamba kuna ajali imetokea maeneo ya Boko CCM ambapo
alienda kutekeleza wajibu wake ikiwa ni pamoja kupima jinsi ajali
ilivyotokea.
“Askari
huyo alipofika eneo la tukio alikuta gari la Lugenge lenye namba za
usajili T 181 DMM aina ya Mark II Grande limegonga kwa nyuma gari namba T
347 CAR Toyota Rav 4 lililokuwa likiendeshwa na James Mushi ambaye
alimtaka Lugenge waende kituoni kutoa maelezo pia kupimwa kama alikuwa
amelewa,” kilisema chanzo.
Kiliendea
kudai kwamba gari la kuvuta magari ‘break down’ lilifika katika eneo
hilo lakini Wakili Lugenge ambaye zamani alikuwa polisi mwenye cheo cha
mkaguzi aligoma kwenda kituoni.NA GPL
...Gari la wakili kwa nyuma.
Imeelezwa
kwamba vurumai ikaanza ambapo wote walidondoshana chini, Leon alimuona
Lugenge akichomoa bastola kiunoni akitaka kumpiga risasi lakini aliwahi
kumgonga mkono kisha bastola ikadondoka chini.
Taarifa
zaidi zinaeleza kwamba Leon aliiwahi ile silaha na kumwamuru Lugenge
atii amri ambapo alinyosha mikono juu ila alikataa kwenda kituoni ndipo
askari yule aliamuru gari livutwe hadi Kituo cha Polisi Wazo Hill na ile
bastola akaikabidhi kituoni hapo.
Imeelezwa kwamba tayari Lugenge anashikiliwa kituoni hapo na Leon alikwenda kutibiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura alipoulizwa juu ya sakata hilo alikiri kuwepo.
“Lugenge
tunamshikilia kwa upelelezi na wakati wowote tutamfikisha mahakamani
tukimaliza uchunguzi wetu. Sikutegemea wakili kufanya kitendo hicho
kibaya,” alisema Kamanda Wambura.
No comments:
Post a Comment