Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, July 15, 2013

WAREMBO MPO.. KUTANA NA 'SNAIL FACIAL'(KONOKONO WANATUMIKA)


Konokono akipita katika paji la uso la mmoja wa wateja katika saluni itoayo huduma hiyo nchini Japan.
Mhudumu wa Saluni ya Ci:z.Labo akimpatia huduma ya 'Snail Facial ' mteja wake. (Picha na AFP/Getty Images)
KUWEKEWA konokono katika paji la uso wako kwa ajili ya urembo inaweza kuonekana kama jambo la ajabu, lakini nchini Japan imekuwa jambo la kawaida na wanawake wamekuwa wakipatiwa huduma hiyo.
Wanawake na akina dada wanaopenda ngozi zao kuwa nyororo, kuondoa mikunjo na uchafu  hutembelea katika saluni ya Ci:z.Labo ambayo hutoa huduma hiyo ya kutengeneza ngozi kwa kutumia konokono 'Snail Facial '.
Mmoja wa wafanyakazi katika saluni hiyo, Manami Takamura anaeleza kuwa uterezi anaouacha konokono katika ngozi huondoa seli za zamani, hutibu ngozi baada ya kuunguzwa na jua pamoja na kuilainisha.
Huduma hiyo kwa saa moja inagharimu kiasi cha pauni 161 ambazo ni sawa na shilingi 392,951 za Kitanzania. Kwa kiasi hicho mteja uanza kwa kuoshwa kabla ya konokono hao kupitishwa katika uso wake. Baadaye hufuata huduma nyinginezo zianazoambatana na utengenezaji wa ngozi.
Baadhi ya wateja waliopata huduma katika saluni hiyo wanasifia huduma hiyo na kuwa imefanya ngozi zao ziwe nyororo na za kuvutia.

No comments:

Post a Comment