Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, July 15, 2013

Ziara ya Spika wa Bunge la Korea Nchini Tanzania

7
Spika  wa Bunge la Jamhuri ya Korea Kusini wiki iliyopita alihitimisha  ziara ya siku tatu hapa nchini aliyoianza tarehe 8 hadi 10 Julai 2013 ambapo alikutana na viongozi wakuu wa Taifa. Awali alikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda. Spika huyo pia akiambatana na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai aliizuru Zanzibar na kukutana na  Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mohammed Shein na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. A.P. Kificho. Katika mazungumzo waliyofanya, jambo lililojikeza na kupokelewa kwa mtizamo chanya ni lile la Tanzania kufungua Ubalozi nchini Korea. Pichani Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda wa nne kushoto na Spika wa Bunge la Korea Mhe. Kang Chang-Hee wa nne kulia wakiendesha mkutano baina yao na wabunge wa nchi zote mbili ulifanyika jijini Dar es Salaam. 6Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein (kulia) akiwa na mazungumzo na Spika wa Bunge la Korea Kusini Mhe. Kang Chang-Hee (kushoto). Katikati ni mkalimani. 5Spika Kang akipokelewa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. A.P. Kificho mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Zanzibar. 4   Spika Makinda akimkabidhi mgeni wake zawadi mara baada ya chakula cha jioni. 3Picha ya pamoja ya viongozi hao baada ya mkutano ambao baadhi ya mambo yaliyozungumziwa ni pamoja na Korea kuuwekeza hapa nchini katika Nyanja ya TEHAMA. 2Wajumbe wa mkutano kwa upande wa Tanzania. 1Spika wa Bunge la Korea Kusini Mhe. Kang Chang-Hee akiushukuru ujumbe wa Tanzania kwa heshima kubwa mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini. (Na Prosper Minja – Bunge)8Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) wakati wa ziara ya Spika wa Korea visiwani Zanzibar.
8Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) wakati wa ziara ya Spika wa Korea visiwani Zanzibar

No comments:

Post a Comment