Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, August 26, 2013

AFANDE SELE,YUKO HOI HOSPITAL AKISUMBULIWA NA MALARIA GET WELL SOON RASTA


 Msanii waMuziki Seleman Msindi Afande Sele  amelazwa katika kituo cha Afya cha Uluguru kilichopo mtaa wa Karume Morogoro  akisumbuliwa na  Malaria kali na Homa ya Matumbo .Akizungumza  mke wa msanii huyo wa muziki wa bongofleva nchini Bi Asha Msindi alisema  mumewe alikumbwa na maradhi hayo alhamisi iliyopita na kwamba baada ya hali kuwa mbaya siku iliyofuata[ljumaa]walimkimbiza kwenye kituo hicho cha afya na kulazwa .

 Vipimo vimeonyesha ana Malaria kali na Homa ya matumbo ambayo ndio inayosababisha kutapita mara kwa mara ili kukabiliana na hali hiyo amemtundikia dripu  kumuongeza nguvu.


  Dr kiongozi wa kituo hicho Dr Kashakya Rubagunya alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi alisema  wamempokea msanii huyo ijumaa iliyopita na kwamba baada ya kumpima wamegundua  anasumbuliwa na Malaria kali,na Homa ya matumbo.

No comments:

Post a Comment