Msichana
mmoja ambaye jina lake halikujulika amejikukuta katika wakati mgumu
baada ya kuzomewa na kuchapwa viboko na kundi la watu katika eneo la
soko la nmc jiji arusha kwa madai ya kuvaa nguo fupi hali iliyowalazimu
wasamariawema kuingilia kati na kutumia nguvu kubwa ili kumwokoa na
kumsitili kwa kumfunika na nguo zingine.
Mwandishi wetu Halfani Lihundi kutoka arusha
alikuwapo katika sakata hilo na ametuma taarifa hii iliyosema, watu
walio shuhudia tukio hilo wamesema wamechukizwa na aina ya nguo
alizizovaa msichana huyo ambazo haziendani na maadili ya Kitanzania,
ndiyo maana wameamua kumwadabisha ili kukomesha tabia hiyo.
Kwa upande wao wanawake waliyo msitili msichana huyo
kwa kumpa nguo za heshima na kumhifadhi katika Gareji ya jirani kabla ya
kumkimbiza kwa gari aina ya Toyota Hiace wamesema hawaridhishwi na
tabia hiyo inayowazalilisha wanawake na kuwataka wasichana kuavaa nguo
za kujisitili ili kujenga heshima katika jamii.
Source ITV
No comments:
Post a Comment