Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imebandika
rasmi kwenye ubao wa matangazo majina ya waombaji uongozi kwenye
uchaguzi wa TFF na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ilikutoa fursa kwa pingamizi.
Kipindi
cha pingamizi kinaanza kesho (Agosti 24 mwaka huu) hadi sas 10 kamili
jioni ya Agosti 26 mwaka huu ambapo waweka pingamizi wanaruhusiwa
kupitia taarifa za wale wanaokusudia kuwawekea pingamizi kabla ya
kuwasilisha pingamizi husika.
Kwa
mujibu wa tangazo la uchaguzi, Agosti 27 hadi 29 mwaka huu ni wawekaji
pingamizi na wawekewa pingamizi kufika mbele ya Kamati ya Uchaguzi kwa
ajili ya kusikiliza pingamizi.
Waombaji
kuwania uongozi katika TFF ambao majina yao yamebandikwa ni Athuman
Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi, Omari Mussa Nkwarulo na Richard J.
Rukambura (urais). Nafasi ya Makamu wa Rais ni Imani Omari Madega,
Ramadhan Omari Nassib na Walace John Karia.
Walioomba
nafasi za ujumbe kuwakilisha kanda ni Kanda Namba Moja (Kagera na
Geita) ni Abdallah Hussein Mussa na Kaliro Samson. Kanda Namba Mbili
(Mara na Mwanza) ni Jumbe Odessa Magati, Mugisha Mujwahuzi Galibona,
Samwel Nyalla na Vedastus Kalwizira Lufano.
Kanda
Namba Tatu (Shinyanga na Simiyu) ni Epaphra Amana Swai, Mbasha Matutu
Mong’ateko na Stanslaus Haroon Nyongo. Kanda Namba Nne (Arusha na
Manyara) ni Ally Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omari Walii Ali.
Kanda
Namba Tano (Kigoma na Tabora) ni Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamisi
Kitumbo. Kanda Namba Sita (Katavi na Rukwa) ni Ayoub Nyaulingo, Blassy
Mghube Kiondo, Nazarius A.M. Kilungeja. Kanda Namba Saba (Iringa na
Mbeya) ni Ayoub Shaibu Nyenzi, Cyprian Charles Kuyava, David Samson
Lugenge, Elias Lusekelo Mwanjala, Eliud Peter Mvella na John
Mwachendang’ombe Kiteve.
Waombaji
wa Kanda Namba Nane (Njombe na Ruvuma) ni James Patrick Mhagama,
Kamwanga Rajabu Tambwe na Stanley William Lugenge. Kanda Namba Tisa
(Lindi na Mtwara) ni Athuman Kingome Kambi, Francis Kumba Ndulane na
Zafarani Mzee Damoder.
Kanda
Namba Kumi (Dodoma na Singida) ni Charles Komba, Hussein Zuberi Mwamba
na Stewart Ernest Masima. Kanda Namba 11 (Morogoro na Pwani) ni Farid
Salum Mbarak, Geoffrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma
Majala na Twahil Twaha Njoki.
Wanaowania
kuteuliwa kugombea kupitia Kanda Namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) ni
Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed wakati Kanda Namba 13 (Dar
es Salaam) ni Alex Chrispine Kamuzelya, Muhsin Balhabou, Omar Isack
Abdulkadir, Shaffih Dauda Kajuna na Wilfred Mzigama Kidao.
Kwa
upande wa TPL Board waliotangazwa kuomba kuwania uongozi wa juu ni
Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti) na Said Muhammad Said Abeid (Makamu
Mwenyekiti).
Wajumbe
wa Kamati ya Uendeshaji ni Kazimoto Miraji Muzo, Michael Njunwensi
Kaijage, Omari Khatibu Mwindadi, Salum Seif Rupia na Silas Masui
Magunguma.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment