Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Mbeya
MAAFANDE
wa jeshi la Magereza, Tanzania Prisons maarufu “Wajelajela”
wamesikitishwa na kufanya vibaya mechi mbili za kwanza ligi kuu soka
Tanzania bara, lakini wamekiri chanzo cha kilio chao ni kukosa uzoefu
kwa mlinda mlango wao namba mbili Ibrahim Shaban baada ya kipa namba
moja, Mweta kuumia na kusababisha kufungwa kirahisi, huku nao mabeki
wakicheza chini ya kiwango.
Prisons
alianza ligi kwa kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika
uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani, na hapo jana katika dimba hilo
walilala kwa bibi kwa kufungwa mabao 3-0 mbele ya JKT Ruvu na sasa
wapo mkiani mwa msimamo wa ligi kuu.
Kocha
wa klabu hiyo, Jumanne Chale amesema amekaa chini na kutathimini hali
ya kikosi chake na sasa anafuta makosa ya vijana wake kabla ya kuwavaa
wakali wa Tang, Coastal Union mnamo septemba 14 mwaka huu uwanja wa CCM
Mkwakwani jijini Tanga, “waja leo waondoka leo”, ambao hapo jana
waliwabana Yanga kwa kutoka sare ya 1-1.
Chale
ameongeza kuwa kupoteza mechi mbili za mwanzo sio kwamba wamepotea,
bali kuna mechi nyingi sana zinazokuja, hivyo wanajipanga upya kwa
kuanzia na mechi ya wagosi wa Kaya.
“Mashabiki
weye roho nyepesi wanaona kama hatuwezi, nawakumbuka mashabi wetu wa
Mbeya kuwa tuna nafasi ya kujipanga vizuri, na waondoe shaka kwani
tumekaa chini na kuangalia namna ya kuimarisha kikosi”. Alisema Chale.
Naye
katibu mkuu wa klabu hiyo, Sadick Jumbe amesema kwa sasa timu itaendelea
kuwepo Magereza ya Ukonga jiini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa
Coastal Union na kikosi kitaondoka septemba 10 kuelekea Tanga.
“Kikosi
kipo salama, tumepoteza mechi, lakini ni kawaida sana katika soka, sio
muda muafaka wa kukata tama, bado tunao muda mzuri wa kusahihisha makosa
na kufanya mambo makubwa sana”.Alisema Jumbe.
Jumbe
amesema kuburuza mkia kwa mechi mbili tu si kigezo cha kuwaona maboya
msimu hu, bali wanajipanga vikali mno kuhakikisha wanawapa shughuli
nzito wapinzani katika mechi zijazo.
Msimu
uliopita Tanzania Prisons ilimaliza katika nafasi ya 9 na ilipigana
sana kukwepa mkasi wa kushuka daraja, na msimu huu mpaka sasa wanaburuza
mkia kwa kutokuwa na pointi yoyote kibindoni.
No comments:
Post a Comment