RPC Ramadhan Mungi.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, wabunge Tundu Lissu, Peter Msigwa, Joseph Mbilinyi (Sugu), David Silinde na viongozi wengine wa mkoa na Wilaya ya Iringa mjini, akiwemo Diwani Nyalusi, wamekamatwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu Iringa na kuhojiwa kwa masaa matatu.
Viongozi hao walikamatwa majira ya saa 3 asubuhi katikati ya mji wa Iringa wakati wakitokea eneo la Kihesa kuelekea Bungeni mjini Dodoma kwa shughuli za kibunge.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, wabunge Tundu Lissu, Peter Msigwa, Joseph Mbilinyi (Sugu), David Silinde na viongozi wengine wa mkoa na Wilaya ya Iringa mjini, akiwemo Diwani Nyalusi, wamekamatwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu Iringa na kuhojiwa kwa masaa matatu.
Viongozi hao walikamatwa majira ya saa 3 asubuhi katikati ya mji wa Iringa wakati wakitokea eneo la Kihesa kuelekea Bungeni mjini Dodoma kwa shughuli za kibunge.
Akithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao ,
kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi amesema kuwa viongozi
hao walikamatwa kwa mahojiano kutokana na kutoa kauli hatarishi kwa amani
ya Tanzania wakati wa mkutano wao uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa kwa ajili
ya mabaraza ya ukusanyaji wa maoni ni rasmu ya katiba.
Kamanda Mungi amesema kuwa kibali
ambacho Chadema walipewa kilikuwa kikianza saa 9 Alasili hadi saa 12 :00
ila wao waliendelea na mkutano huo hadi majira ya saa 12 .25 na kila
walipofuatwa zaidi ya mara moja kuelezwa kuhusu muda wa kibali chao
kuisha bado viongozi hao waliendelea kuendesha mkutano huo huku wakitumia
vipasa sauti kutoa maneno ya dhahaka dhidi ya jeshi la polisi.
Hata hivyo Mungi amesema kuwa jeshi la
polisi lilishindwa kutumia nguvu kuwakamata ama kuwashusha viongozi
hao jukwaani wakati wa mkutano huo kama njia ya kuepusha vurugu ambazo
zingeweza kutokea iwapo nguvu zingetumika kuwashusha kwa kuvunja sheria
za nchi .
"Tunawashikilia viongozi hao kutokana
na kutoa kauli hatarishi wakati wa mkutano wao wa jana (juzi)
uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa ...
"Kibali chao kilikuwa kikiisha
saa 12 .00 jioni ila wao walizidisha muda na maofisi wa polisi
waliokuwepo waliwafuata na kuwakumbusha juu ya muda waliopewa katika kibali
chao ila wao badala ya kusitisha mkutano walitumia kipasa zauti kujibu na
kutoa kauli cha hatarishi ....
"Jeshi la polisi lilitumia busara na kuwaacha
hadi walipomaliza na asubuhi tuliwakamata kitaalam bila ya kutokea vurugu
zozote" Mungi
Amesema kuwa viongozi hao hadi
majira ya saa 5 leo asubuhi
walikuwa wakiendelea kuhojiwa na jeshi la polisi na kuwa kufikishwa ama
kutofikishwa mahakamani kutajulikana mara baada ya mahojiano hayo .
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya
Iringa Suzana Mgonakulima alisema kuwa jumla ya waliokamatwa jana ni
viongozi wanne akiwemo Mbowe, mbunge Msigwa , Lissu pamoja na diwani wa kata
ya Mvinjeni katika Manispaa ya Iringa Frank Nyalusi .
Kuhusiana na kumamatwa na kuachiwa kwa
viongozi hoa amesema kuwa viongozi hao waliachiwa majira ya saa 5.30 asubuhi
baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya masaa matatu ambapo kila mmoja alitakiwa
kudhaminiwa na mtu mmoja kwa dhamana ya Tsh milioni 2 na wote walikidhi
masharti ya dhamana na kuruhusiwa kuendelea na safari hadi hapo
watakapotakiwa kufika polisi .
Credit: Matukio daima
Credit: Matukio daima
No comments:
Post a Comment