Mtandao wa Sky Sports umesema vyanzo vyake vya kuaminika vya habari vimeuambia mtandao huo kwamba Tottenham wanafikiria kukubali
ofa kutoka kwa klabu kadhaa kwa ajili ya Gareth Bale - na kusisitiza
kwamba bado hawajakubaliana na Real Madrid kumuuza winga huyo.
Ripoti nchini Spain wikiendi hii zilikuwa zikisema kwamba Madrid walikuwa wanamalizia taratibu za mwisho za kumsaini Bale katika dili ambalo lingevunja rekodi ya dunia - huku Spurs wakiripotiwa kukubali kumuuza nyota huyo.
Japokuwa, sasa imefahamika hakuna makubaliano yaliyofikiwa baina ya Tottenham na Real na sasa klabu hiyo ya White Hart Lane inafikiria ofa za klabu nyingine.
Manchester United wamekuwa wakitajwa kuvutiwa na Bale, lakini inabaki kusubiriwa kama David Moyes ndio kocha mwingine aliyejiingiza katika mbio za kumtaka winga huyo mwenye miaka 24.
No comments:
Post a Comment