Chaz na mkewe kwenye misa.
Wakionyesha vyeti vyao vya ndoa.
Baada ya misa wakiwa na furaha kuu.
RAIS wa bendi ya Mashujaa, Charles Gabriel Cyprian ‘Chaz Baba’, juzikati aliua ndege wawili kwa wakati mmoja pale alipotoa burudani ya nguvu katika sherehe ya harusi yake iliyofanyika katika ukumbi wa Mirado Hall uliopo Sinza Makaburini jijini Dar, na pia kutinga katika ukumbi wa Mango Gadern Kinondoni jijini Dar ambapo Twanga Pepeta walikuwa wakiendeleza wimbi la burudani katika ukumbi huo.
Tukio hilo la Chaz kutinga katika ukumbi wa Mango liliwashangaza wengi kwani kwa wakati ule Chaz alitakiwa kwenda kupumzika kutokana na mkewe kuonekana amechoka kwa sababu ya ujauzito wake.
“Shemeji yetu anaonekana kachoka sana lakini Chaz ndio kwanza anaonekana hana hata muda wa kwenda kulala mapema” alisema shabiki mmoja aliyekuwa ndani ya ukumbi.
Chaz Baba alifunga ndoa na Rehema Sospeter Marwa, siku ya Agosti 24, mwaka huu katika kanisa la St Peters jijini Dar es Salaam.
CHAZ BABA AFUNGA NDOA, ATINGA UKUMBI WA ‘TWANGA’ KUJINAFASI AKIWA PEKE YAKE
Chaz Baba akimpigia simu bi harusi (mkewe) ili awahi misa ya ndoa yao.
Bw. na Bi Deo Mutta waliokuwa wasimamizi wa Chaz Baba.
RAIS wa bendi ya Mashujaa, Charles Gabriel Cyprian ‘Chaz Baba’,
juzikati aliua ndege wawili kwa wakati mmoja pale alipotoa burudani ya
nguvu katika sherehe ya harusi yake iliyofanyika katika ukumbi wa
Mirado Hall uliopo Sinza Makaburini jijini Dar, na pia kutinga katika
ukumbi wa Mango Gadern Kinondoni jijini Dar ambapo Twanga Pepeta
walikuwa wakiendeleza wimbi la burudani katika ukumbi huo.Bw. na Bi Deo Mutta waliokuwa wasimamizi wa Chaz Baba.
Tukio hilo la Chaz kutinga katika ukumbi wa Mango liliwashangaza wengi kwani kwa wakati ule Chaz alitakiwa kwenda kupumzika kutokana na mkewe kuonekana amechoka kwa sababu ya ujauzito wake.
“Shemeji yetu anaonekana kachoka sana lakini Chaz ndio kwanza anaonekana hana hata muda wa kwenda kulala mapema” alisema shabiki mmoja aliyekuwa ndani ya ukumbi.
Chaz Baba alifunga ndoa na Rehema Sospeter Marwa, siku ya Agosti 24, mwaka huu katika kanisa la St Peters jijini Dar es Salaam.
(PICHA /HABARI:SHAKOOR JONGO /GPL)
No comments:
Post a Comment