Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, August 24, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 24. 08. 2013.


WILAYA YA MOMBA – WATU SABA WAKAMATWA KWA KOSA LA KUHARIBU MALI NA KUJERUHI.
MNAMO TAREHE 21.08.2013 MAJIRA YA  SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MCHANGANI KIJIJI CHA SENGA KATA YA  KAMSAMBA WILAYA YA  MOMBA MKOA WA MBEYA.  KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KUTOKA KATIKA KIJIJI CHA ILAMBO KATA YA  KAPETA WILAYA YA  SUMBAWANGA VIJIJINI MKOA WA RUKWA WALIVAMIA MAKAMBI YA  WAVUVI YALIYOPO KATIKA KIJIJI HICHO NA KUWAPIGA KWA KUTUMIA FIMBO KISHA KUCHOMA MOTO MABANDA KADHAA YA  WAVUVI YALIYOJENGWA KWA KUTUMIA NYASI.
CHANZO CHA TUKIO HILO NI KUGOMBEA  ENEO LA VIJIJI TAJWA. UFUATILIAJI WA MGOGORO HUU UNAENDELEA.  JUMLA YA  WATU SITA WALIJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO AMBAO NI 1. MSABAHA S/O JUMA, MIAKA 40, MZARAMO,MKULIMA/MVUVI  2. MAXIMO S/O MWAKANYEMBA, MIAKA 24,KYUSA,MKULIMA/MVUVI  3. MICHAEL S/O SANGA, MIAKA 30,MKINGA,MKULIMA/MVUVI 4. CHONDE S/O KALISTO, MIAKA 56, MNYAMWANGA, MKULIMA/MVUVI 5. ZAWADI S/O JOHN SICHULA, MIAKA 39, MNYAMWANGA, MKULIMA/MVUVI NA 6. GIBSON S/O EDWARD KACHINGWE, MIAKA 26, MSAGALA, MKULIMA/MVUVI WAHANGA WOTE NI WAKAZI WA KIJIJI CHA SENGA NA WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.
 KUFUATIA TUKIO HILO JUMLA YA  WATUHUMIWA SABA WAMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI AMBAO NI 1. SAMWEL S/O DAUD, MIAKA 42, MNYIHA,  MKULIMA 2. GERVAS S/O LUKAS, MIAKA 52, MSUKUMA, MKULIMA 3.NYERERE S/O MWITA,  MIAKA 52,MSUKUMA,MKULIMA 4.RICHARD S/O WILSON, MIAKA 43, MFIPA, MKULIMA 5. GEBRUS S/O RAMADHAN, MIAKA 28, MNYASA, MKULIMA 6. LULINDE S/O DASE, MIAKA 43, MSUKUMA, MKULIMA NA 7. FUNGUZA S/O MASANJA, MIAKA 43, MSUKUMA, MKULIMA WATUHUMIWA WOTE NI WAKAZI WA KIJIJI CHA SENGA KAMSAMBA. KWA SASA HALI NI SALAMA KATIKA ENEO HILO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII  KUTOJICHULIA SHERIA MKONONI NA KUITATUA MIGOGORO YAO KWA NJIA YA  MAZUNGUMZO. AIDHA ANATOA RAI  KWA   YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI WALIPO WATUHUMIWA  WENGINE WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.
WILAYA YA  KYELA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO].
MNAMO TAREHE 23.08.2013 MAJIRA YA  SAA 10:35HRS HUKO KYELA- KATI WILAYA YA  KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA KAMWELA S/O MWASAMWENE,MIAKA 37,KYUSA,MKULIMA,MKAZI WA MBUGANI AKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI UJAZO WA LITA NANE [08] AKIWA AMEBEBA KWENYE BAISKELI YAKE. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.
WILAYA YA  MBEYA MJINI – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MNAMO TAREHE 23.08.2013  MAJIRA YA  SAA 17:30HRS HUKO UYOLE JIJI NA  MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA DEMARK S/O RAFOE,MIAKA 28,RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA  KIFICHO.  TARATIBU ZINAFANYWA ILI AKABIDHIWE IDARA YA  UHAMIAJII. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA KUHUSU WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
                                                        Signed by:
                                                        [ DIWANI ATHUMANI   - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment