Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, August 26, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 26. 08. 2013.



WILAYA YA MBOZIAJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO
MNAMO TAREHE 25/08/2013 MAJIRA YA SAA 09:30 HRS HUKO KIJIJI CHA CHIMBUYA WILAYA YA MBOZI. GARI NO 509 BNP/T 231 BME HORSE FAW LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE RINGO S/O SIJABAJE, MIAKA 34, MSAFWA NA MKAZI WA FOREST MBEYA, LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AITWAYE SAILOSI S/O CHEYO, MIAKA 14, MNDALI, MWANAFUNZI WA S/M CHIMBUYA DARASA LA SITA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO, CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA VWAWA. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVAKUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA PIKIPIKI [BODABODA [KUGONGA GARI KWA NYUMA NA KUSABABISHA KIFO.
MANMO TAREHE 25/08/2013 MAJIRA YA SAA 16:30 HRS HUKO MBALIZI MWAKAPANGALA WILAYA YA MBEYA VIIJINI BARABARA YA TUNDUMA/MBEYA PIKIPIKI NO T.174 BSK AINA YA T/BETTER IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA  MIAKA 20-25 ALILIGONGA KWA NYUMA GARI NO T. 388 BXS/T.183 ABX AINA YA SCANIA SEMI TREILA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE JOSEPH S/O KISINDA, MIAKA 38, MHEHE MKAZI WA  DSM. MWENDESHA PIKIPIKI ALIFARIKI WAKATI AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI  TEULE YA  IFISI, CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA MWENDESHA PIKIPIKI, DEREVA WA GARI AMERIPOTI NA GARI LIPO KITUONI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVAKUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBOZI -   AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA PIKIPIKI NA KUSABABISHA KIFO.
 MANMO TAREHE 25/08/2013 MAJIRA YA SAA 20:45HRS HUKO MAHENJE BARABARA YA MBEYA /TUNDUMA GARI NO T. 561 BAJ AINA YA TOYOTA COSTER LIKIENDESHA NA DEREVA BENARD S/O MLIMBA, LILIMGONGA MPANDA BAISKELI AITWAYE FURAHA S/O MWAIPOPO, MIAKA 26, MNYAKYUSA, DEREVA WA BODABODA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO NA KUMSABABISHIA MAJERAHA KWA ABIRIA AITWAYE NIONE S/O SANGA, MIAKA 27, MKINGA NA MKAZI WA MWAKA TUNDUMA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA VWAWA NA MAJERUHI   ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVAKUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA                                      
Signed by
[ DIWANI  ATHUMANI   - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment