Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 22, 2013

UVCCM WAMPONGEZA RAIS DK. SHEIN kwa kufanya marekebisho katika muundo na majukumu ya baadhi ya Wizara


SONY DSC Naibu katibu Mkuu (UVCCM) Zanziba,Shaka Hamdu Shaka (kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo Agosti 21,2013 , Makao Makuu ya Umoja wa Vijana (CCM) jijini Dar es salaam wakati akitoa pongezi kutoka Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi(UVCCM) kutokana na hatua zilizochukuliwa na Rais wa Zanziba Dk.Ali Mohamed Shein ambaye amefanya mabadiliko ya Baraza lake la Mawaziri na kupangua Idara zilizokuwa zikisimamiwa na Wizara mbalimbali (kulia) Mjumbe Kamati Teule  (UVCCM) Taifa,  Nadra Juma
SONY DSCWaandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza kwa umakini Naibu katibu Mkuu (UVCCM) Tanzania Zanziba,Shaka Hamdu Shaka, leo Agosti 21,2013 
PICHA NA PHILEMON SOLOMON FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
Na Philemon Solomon wa Fullshangwe Dar es salaam
Naibu katibu Mkuu UVCCM Zanzibar,  Shaka Hamdu Shaka amesema Rais Dkt. Shein ni msikivu, makini na hodari wa kusoma alama za nyakati na mabadiliko yake, hivyo amefanya hayo kwa nia nzuri akilenga kuwatumikia wananchi chini ya mfumo wa umoja wa kitaifa.
Ameongeza kuwa UVCCM Zanzibar itashirikiana naye bega kwa bega katika kuhakikisha kuwa anatimiza malengo ya serikali na ilani ya chama cha mapinduzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 Jana amefanya marekebisho katika muundo na majukumu ya baadhi ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kufuatia marekebisho hayo, baadhi ya shughuli za Wizara zimeunganishwa na kuundiwa Wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika wizara nyengine.
Hata hivyo marekebisho hayo hayakuongeza idadi ya Wizara na kwa hivyo zinaendelea kubaki wizara 16.

No comments:

Post a Comment