Daktari Afrika Kweka amenaswa akiwa katika jaribio la kumtoa mimba mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Stella.
Tukio
hilo lilitokea juzikati kwenye chumba kilichopo katika jengo la Chama
cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Makurumla, Magomeni-Kagera, Dar.
Awali,
raia wema wa eneo hilo walituma malalamiko yao wakidai kwamba, Dokta
Kweka amekuwa akifanya ‘mauaji’ hayo ya vichanga waziwazi, hali
inayowakera kupita maelezo.
“Jamani
hapa Magomeni-Kagera kwenye jengo la CCM, Tawi la Makurumla, kuna
daktari anaitwa Kweka anatoa sana mimba, hasa wake za watu, njooni
mumnase.”
Baada ya
kupata taarifa hiyo, uliwekwa mtego ambapo mmoja wa waandishi wetu wa
kike alikwenda kwa Dokta Kweka na kujifanya mwanafunzi wa chuo lakini
ana mimba anataka kuichoropoa.
Mwandishi
huyo aliingia na paparazi wa kiume aliyejifanya ni mpenzi wake aliyempa
mimba hiyo. Ndani ya eneo la tukio walipokelewa kwa bashasha na daktari
huyo ambaye alihitaji shilingi 60,000 kama gharama za kutoa mimba japo
baadaye alikubali kushusha bei hadi shilingi 45,000.
Baadaye
daktari huyo alimchukua mwandishi wetu bila kujua kama hakuwa na mimba
wala kitambi na kumpeleka chumba cha kuchomea sindano ambapo almanusura
mpango mzima uharibike kwa kuwa mwandishi wetu hakupaswa kuruhusu
daktari huyo amchome sindano ambayo ilisadikika kuwa ni ya ganzi.
Hata
hivyo, wakati paparazi wetu akijishauri kuhusu sindano hiyo, ndipo
Stella alifika kwenye zahanati hiyo na kuingia ndani kwa dhumuni la
kutoa mimba.
Alipofika
aliingia moja kwa moja chumbani kwa daktari huyo na kuchoma sindano ya
ganzi bila woga kisha akaingia chumba cha kuchoropolea.
Ilikupata
uhakika kuwa, mwanamke huyo ameingia chumba cha kutolea mimba, ndipo
‘wapenzi’ hao (waandishi wetu) waliwasiliana na wapiga picha wetu
waliokuwa chobingo na polisi ambao walitia timu na kuwanasa.
Daktari
huyo na mteja wake walipelekwa kituo cha polisi na kufunguliwa jalada
la kesi namba MMP/RB/567/2013 kosa likiwa kujaribu kutoa mimba huku
ikibainika kuwa zahanati hiyo ni batili kwa kuwa aliisajili kama
maabara.
Naye
Katibu Mwenezi wa CCM wa tawi hilo, Hashim Kimambe alizungumza na
gazeti hili juzi na kukiri kuwa taarifa za kunaswa kwa daktari Kweka
anazo.
Alisema:
“Hata hivyo, sisi tulikuwa mbioni kumfukuza kwa sababu alipoomba
kupanga hapa alisema anaweka duka la dawa (famasi), baadaye tukashangaa
anaziba watu wanaingia ndani.
“Mbaya zaidi huyu jamaa amekuwa akitumia risiti za CCM katika mambo yake, lazima aondoke kwa kweli, tunamwandikia barua.”NA GPL
No comments:
Post a Comment