KATIKA
hali isiyokuwa ya kawaida mkazi wa Kijiji cha Nyabibuye Kakongo katika
Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Susuluka (16) anadaiwa kujeruhiwa
vibaya usoni na bosi wake, Imani Paulo (36) kwa kung’atwa ng’atwa usoni
na kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje, kama ambavyo
anaonekana pichani.
Tukio
hilo ambalo tunaweza kulifananisha na dunia kuelekea kufika mwisho,
limegusa hisia za watu wengi hasa wakazi wa Kibondo, huku wengine
wakitokwa na machozi kutokana na kuguswa na ukatili ambao amefanyiwa
kijana huyo.Tunaweza kufikiria kuwa tukio hilo ni sinema, lakini Mkuu wa
Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamotto, ameliambia Majira kuwa tukio hilo
limetokea miezi miwili iliyopita.
Akizungumza na Majira katika
mahojiano maalumu, Mwamotto, alisema kuwa kabla ya kijana huyo
kujeruhiwa na bosi wake, alimtuma dukani ili akamnunulie
soda.Aliliambia Majirakuwa baada ya kufika nyumbani alimkuta bosi
wake akiwa amemkaba koo mbwa na kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata
mbwa huyo, alianza kuhema akitoa ulimi nje.
DC
Mwamotto alisema kuwa mtuhumiwa huyo ghafla alianza kuung’ata ulimi wa
mbwa na kisha kumeza vipande jambo lililosababisha mbwa huyo kupiga
kelele kutokana na maumivu.Aliongeza kuwa aliendelea kula vipande vya
ulimi huo wa mbwa hadi alipoumaliza.
“Unaweza
kusema kuwa ni uongo, lakini ni tukio la kweli kabisa kwani mshtakiwa
huyo aliendelea kula ulimi wote wa mbwa, huku kijana huyo akiendelea
kumshangaa bosi wake kutokana na kitendo hicho kilichosababisha mbwa
huyo kufa,”Wakati akiendelea kumshangaa bosi wake ghafla alimrukia na
kumkamata kwa nguvu na kuanza kumng’ata kama mtu anayetafuna hindi la
kuchoma.
“Mshtakiwa
huyo alianza kumtafuna jicho moja na kufuatia jicho la pili na kisha
kumeza vipande vya macho huku akiendelea kumshika kwa nguvu,” alisema DC
Mwamotto wakati wa mahojiano naMajira.
Baada ya kumaliza kitendo hicho alisema kuwa mshtakiwa huyo alianza kumng’ata pua na kisha kumeza na vipande.
Alisema
kuwa wakati anaendelea na kitendo hicho majeruhi huyo alikuwa akipiga
kelele za kuomba msaada, lakini mshtakiwa huyo alianza kumng’ata tena
kipande cha mdomo wa chini na kisha kusababisha meno kubaki
nje.“Kutokana na kelele hizo wananchi waliamua kusogea karibu, lakini
walikuta tayari, Susuluka amejeruhiwa vibaya usoni huku damu zikimtoka
kwa wingi,” alisema.
Mwamotto
alisema kuwa kutokana na hali hiyo wananchi walimvamia na kumpiga na
kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Kibondo na majeruhi walimkimbiza
katika Hospitali ya Wilaya ya Kibondo.
Majira iliendelea
na mahojiano hayo ambapo, mshtakiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya
Wilaya na kufunguliwa mashtaka ya kudhulu mwili.“Hivi sasa mshtakiwa
yupo katika Gereza la Nyamisivi Kibondo, lakini cha kusikitisha tena
akiwa huko alimng’ata na kula vipande vya nyama vya mguu mshtakiwa
mwenzake,” alisema.
Alisema
kuwa mshtakiwa mwenzake alimjeruhi vibaya na kupelekwa hospitalini hali
iliyosababisha mshtakiwa huyo kutengwa na washtakiwa wenzake.“Mimi
nimelazimika kwenda hadi gerezani na kufanya mahojiano na mshtakiwa
huyu, kwani hili tukio linasikitisha sana lakini cha ajabu alitaka
kufahamu je ameshtakiwa kwa makosa gani ya kuua mbwa au kumng’ata mtu,”
alisema.
Alisema
kuwa pia amelazimika kwenda kumjulia hali majeruhi huyo ambapo
madaktari katika hospitali hiyo walishindwa kumtibia.“Nimeomba msaada
kutoka Wizara ya Afya ili mgonjwa
huyu akatibiwe India na tayari maandalizi yameanza kufanyika kwa kushirikiana na Hospitali ya Kibondo,” alisema.
Mwamotto
alisema kuwa mgonjwa huyo hana pua, macho yamefumba, mdomo kwa
kujeruhiwa vibaya usoni hali ambayo anahitaji matibabu zaidi.Amewaomba
Watanzania kumsaidia kijana huyo ili aweze kwenda kutibiwa haraka nje
pamoja na kupata msaada mbalimbali kwa kuwasiliana na mganga mkuu wa
hospitali ya Kibondo ama kuwasiliana na Mhariri mtendaji wa gazeti laMajira
Habari hii kwa hisani ya gazeti la majira la Tanzania.
No comments:
Post a Comment