Ruhila Adatia-Sood
Ruhila, alikuwa katika ghorofa ya juu ya duka la Westgate ambako alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wameandaa mashindano ya upishi kwa watoto.
Alikuwa ameolewa na Ketan Sood, aliyefanya kazi na shirika la USAid mjini Nairobi mwezi Januari mwaka 2012,na harusi yake ilitajwa kuwa harusi ya kiswahili ambayo ilisherehekewa kwa siku tatu.
Alikuwa mjamzito na mimba ya miezi sita alipofariki.
Kulingana na ripoti Adatia-Sood alikimbizwa hospitalini , lakini alifariki baada ya kuwasili kutokana na kuvuja damu nyingi.
Alisifika kote nchini kwa moyo wake mzuri wa kuwafanya watu kutabasamu daima.
Alisomea katika chuo kikuu cha Rhodes nchini Afrika Kusini , na dada zake watatu wamemtaja kama mtu mwenye ari kubwa maishani.
Pia alikuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha East FM na pia alitangaza habari kwenye kituo cha televisheni ya Kiss.
Magaidi waliwarushia magurunedi Rahila na mtangazaji mwenzake pamoja na watoto waliokuwa ndani ya jengo hilo lakini Ruhila hakuponea. Mwenzake Kamal Kaur, pia mtangazaji wa redio alikuwa ameambatana na watoto wake ambao walifyatuliwa risasi ingawa ziliwakosa na kumgonga mtoto aliyekuwa karibu nao. Wao walijeruhiwa miguuni.
Kaur na wanawe walifanikiwa kukimbilia usalama wao.
Mbugua Mwangi and Rosemary Wahito
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pia aliwapoteza jamaa zake katika shambulizi hilo. Mbugua Mwangi ni mpwa wa Kenyatta na alikuwa na mchumba wake Rosemary Wahito wakati waliposhambuliwa kwa risasi na kuuawa papo hapo.Akihutubia taifa, Kenyatta alisema kuwa, "ninamuomba Mungu awape utulivu wakati sote tukikumbwa na msiba huu na ninajua mnachokihisi hasa ikiwa umempoteza jamaa wako katiakshambulizi hili baya.''
Kulingana na taarifa ya jarida la nchini Ireland, mamake Mwangi, Catherine Muigai Mwangi, ndio alikuwa tu amerejea kutoka Dublin ambako alikuwa balozi wa Kenya kwa miaka sita .
Dadake mkubwa Rais Kenyatta Christine Wambui Pratt pia alikuwa katika jengo hilo lakini alifanikiwa kunusuru maisya yake.
Mitul Shah
Afisaa mkuu mtendaji wa mauzo katika kampuni ya Bidco, ambayo hutengeza mafuta ya kupikia, Mitul Shah alikuwa katika ghorofa ya juu zaidi ya jengo hilo.
"Alifariki akijaribu kuwaokoa watoto waliokuwa wamekwama ndani ya jengo hilo. Kwa marafiki wa Mitul, alifariki kama shujaa .
Rafiki zake wamemtaja kama shabiki sugu wa Manchester United.
Pia alikuwa mwenyekiti wa timu ya soka ya Bidco.
Joyti Kharmes Vaya na Maltiben Ramesh Vaya ambao ni wifi
Maltiben Ramesh Vaya alikuwa na miaka 41 , mama wa watoto wawili aliyefanya kazi katika Benki ya Baroda.
Wawili hao walikufa kutokana na majeraha waliyopata, kutoka na risasi
Kofi Awoonor
Alikuwa mjini Nairobi kushiriki hafla ya Storymoja na alitarajiwa kutumbuiza watu siku ya Jumamosi.
Alisifika kwa nyimbo na mashairi yake mapema miaka ya sitini.
Miaka ya sabini alifunza katika baadhi ya vyuo vikuu nchini Marekani na kurejea Ghana mwaka 1975 kuchukua wadhifa wa mwalimu wa lugha ya kiingereza katika chuo kikuu cha Cape Coast.
Katika muda wa miezi kadhaa, alikamatwa na kuzuiliwa kwa madai ya njama ya uhaini wakati wa utawala wa kijeshi wa Kanali Ignatius Acheampong.
Mwanawe Awoonor alikuwa naye wakati wa shambulii hilo mjini Nairobi na alipigwa risasi mkononi wakati wa shambulizi hilo.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment