Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, September 24, 2013

UPDATES: SHAMBULIO LA KIGAIDI NCHINI KENYA -Mateka wote wadaiwa kuokolewa -Vikosi vya usalama vinakamilisha zoezi la kudhibiti jengo zima la Westgate -Idadi ya magaidi waliouawa ni sita


Baadhi ya wanausalama wakiwa nje ya jengo la Westgate jijini Nairobi.
-Mateka wote wadaiwa kuokolewa
-Vikosi vya usalama vinakamilisha zoezi la kudhibiti jengo zima la Westgate
-Idadi ya magaidi waliouawa ni sita
-Milio ya risasi ilisikika leo asubuhi, mchana kutoka ndani ya jengo
TAARIFA kutoka serikali ya Kenya zinadai kuwa mateka wote waliokuwa wanashikiliwa na magaidi katika jengo la Westgate wameokolewa.
Vikosi vya usalama nchini humo vinadai kuwa viko katika hatua za mwisho kukamilisha zoezi la kudhibiti jengo zima la Westgate. Magaidi wapatao sita wanadaiwa kuuawa usiku wa kuamkia leo.
Lakini taaria kutoka shirika la AFP zinadai kuwa majeshi ya Kenya yangali yanakabiliana na baadhi ya magaidi ambao wamesalia ndani ya jengo la hilo.
Inadaiwa kuwa magaidi hao walijitawanya ndani ya jengo hilo kila mmoja akijificha sehemu yake katika ghorofa ya juu za jengo hilo.
Katika shambulio hilo lililotokea Jumamosi iliyopita, watu 62 wanadaiwa kupoteza maisha wakati 175 wakijeruhiwa japo kuna taarifa kuwa idadi ya waliokufa ni 69 mpaka sasa. Katika shambulio hilo, mwanamke Samantha Lewthwaite anadaiwa kuwa miongoni mwa magaidi 10-15 waliohusika.

No comments:

Post a Comment