Kiongozi wa kundi la M23 Bertrand Bisimwa amesema kwamba wapiganaji wake wanaondoka kwenye maeneo yao katika kijiji cha Kanyaruchinya , karibu na Goma kwenye mpaka wa Congo na Rwanda ili kuruhusu uchunguzi ufanyike kuamua nani hasa alihusika.
Naye msemaji wa majeshi ya serikali FARDC Olivia Amuli amesema kwamba wanajeshi wa serikali wamerudisha nyuma wapiganaji wa M23 jana na M23 wameondoka kwasababu ya kupata pigo kubwa aliongeza kuwa baada ya mapambano ya siku 9 hatimaye wamedhibiti maeneo ya Kibati na Kilimanyoka na kusema waasi hao wamekimbia huku wakiwa wameacha magari yao yaliopigwa na mabomu.
Wakati huo huo msemaji wa jeshi la Congo alieleza kwamba M23 wamepiga mabomu huko Goma na nchini Rwanda ili wapate usaidizi wa Rwanda huko Congo na sasa wameondolewa huko Kibati akidai kuwa M23 wanadanganya wananchi.
No comments:
Post a Comment