Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza
Mbunge wa CHADEMA jimbo la Maswa Magharibi Mh. John Shibuda wakati
akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya
Meatu mjini Meatu, ambapo ameelezea kuwa Siasa siyo ugonvi na alikuja
Meatu kwa sababu mbili tu Moja ilikuwa ni kukutana na Ndugu Kinana kwa
ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali juu ya tatizo la zao la Pamba
kuhusu bei ya zao hilo na matatizo ya pembejeo kwa wakulima wa Wilaya
hiyo, Akongeza kwamba jambo lia pili ni kwamna Ndugu Abdulrahman Kinana
ni rafiki yake wa muda mrefu kwa hata wakati wakisoma shule wote
walisoma moshi Abdulrahman Kinana akisoma Old Moshi Sekondari na John
Shibuda Mwenyewe akisoma Moshi Technical lakini pia akasema wakati
alipokuwa akigombea ubunge wa Maswa Magharibi Kinana alimchangia
shilingi Milioni moja “Siasa nia Siyo Matusi ni Ushirikiano na kukosoana
kwa hoja” amemaliza Shibuda.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MEATU
SIMIYU) Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza
jambo katika mkutano huo huku Mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi John
Shibuda akimsiliza, kushoto anayetabasam ni Katibu wa NEC Itikadi,
Siasa na Uenezi Nape Nnauye.
Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akizungumza katika
mkutano huo kushoto ni John Shibuda Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi
CHADEMA.
Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akikumbatiana kwa
furaha na John Shibuda Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi CHADEMA mara
baada ya kupanda jukwaani katika viwanja vya Meatu mjini, kushoto ni
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuhudia. Mbunge
wa Jimbo la Maswa Magharibi CHADEMA Mh John Shibuda akiwasili katika
mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya
Meatu mjini Meatu leo huku vijana wa Chama chaCHADEMA wakimsindikiza.. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu8 Abdulrahman Kinana akiwahutubia wana Meatu katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mjini Meatu. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu8 Abdulrahman Kinana akielekea jukwaani mara baada ya kusimikwa Chifu Kilabanya wa wasukuma wa Meatu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipunga usinga juu mara baada ya kusimikwa Chifu Kilabanya wa Wasukuma wa Meatu katika
mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Meatu. kulia ni Mayanga Kidoyayi
Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti (Chifu Kishosha) kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dr Titus Kamani, Nape
Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM na Fale Miungumale. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimikwa na Mzee
Fale na mama Kwimba Tobongo katika kutano wa hadhara uliofanyika
katika viwanja vya Meatu leo jioni aliyeshika kipaza sauti ni Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi CCM na kushoto ni Dr
Titusi Kamani mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa mgolole mweusi kama ishara ya kusimikwa kuwa chifu Kilabanya wa wasukuma wa Meatu. Mlemavu
Daud Deus akikabidhiwa baiskeli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana katika kutano wa hadhara uliofanyika mjini Meatu Simiyu leo
Baiskeli hiyo imetolewa na Salim mmoja wa wana CCM wa Meatu. Daud Deus akijaribu kuendesha baiskeli yake mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo Katibu
wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza na wanaMeatu katika mkutano
wa hadhara uliofanyika viwanja vya Meatu leo mkoani Simiyu.
PIGA MSHINDO WA MAANA NA MERIDIANBET LEO
-
Leo hii mechi zote za kufuzu kwa Afcon zinaenda kumalizika ambapo kuna timu
ambazo tayari zimeshafuzu na zingine bado. Tanzania itakuwa kibaruani leo
kus...
3 hours ago
No comments:
Post a Comment