Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo, aliyefarika Nchini Congo, akiwa katika Jeshi la Kulinda Amani.
Ndege iliobeba Mwili wa Marehemu Meja
Hatibu Shaban Mshindo ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Abeid Amani Karume, Zanzibar ikitokea Dar-es-Salaam.
Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar na
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar
wakijumuika na Ndugu na Jamaa kuupokea mwili wa marehemu Meja Hatibu
Shaban Mshindo.ulipowasili Zanzibar kwa mazishi Kijijin kwao Fujoni kwa
mazishi jioni hii.
Ofisa wa JWTZ akitowa maelezo ya ratiba
ya kuupokea Mwili wa Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo katika uwanja
wa ndege wa Zanziba leo mchana na kuzikwa katika Kijiji cha Fujoni
Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Mjane wa Marehemu na Watoto wake
wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume leo
mchana wakitokea Mjini Dar-es- Salaam.
WANAJESHI wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania wakiwa na mwili wa Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo, baada
ya kuuteremsha katika ndege maalum ya Jeshi.
Wanajeshi wa JWTZ wakitembelea kwa
mwendo wa pole wakiwa na Mwili wa Marehemu Hatibu Shaban Mshindo, baada
ya kuwasili Zanzibar, tayari kwa mazishi yanayofanyika jioni hii katika
Kijiji cha Fujoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Wananchi wakiwa katika viwanja vya ndege
vya Zanzibar wakiupokea mwili wa marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo,
aliyefariki Nchini Congo akiwa katika Jeshi la Kimataifa la kulinda
Amani Nchi Congo.
Msafara wa Magari ya JWTZ ukiondoka
katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kuelekea
katika Msikiti wa Bezredi Muembeladu kwa kuusalia na maziko
yatakayofanyika katika Kijiji chao Fujoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja,
saa kumi jioni.
Na Zanzi Newz