Janne Rajpar mwenyekiti mwenza kwa upande wa wahisani katika kusimamia matumizi ya fedha za umma kutoka ujerumani.
Kutoka
kushoto ni Bi Ingiahedi Mduma ,ambaye ni Mkuu wa kitengo cha
Mawasiliano serikalini, wakatikati ni Bi. Hannah Mwakalinga kutoka PPRA
ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za kiushirikiano na wakushoto kwake ni
Bw. Malima Nkilijiwando ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Mipango kutoka Kwa
Mkaguzi mkuu wa Mahesabu, wakisikiliza kwa makini mada na maoni
yaliyokuwa yakitolewa katika mkutano huo
Wa
kwanza kushoto ni Bw. Sebastian Ndandala ambaye ni Kaimu msimamizi wa
mradi wa maboresho ya fedha za umma( PFMRP) kwa upande wa serikali na
anayefuata ni Bi. Paddy Siyanga Knudsen ambaye ni msimamizi kwa upande
wa Washirika wa maendeleo,wakisikiliza kwa makini mada na maoni
yaliyokuwa yakitolewa katika kikao hicho
Juma
Salumu Maguru Mkurugenzi Msadizi idara ya Mipango Wizara ya fedha
akitoa utangulizi kwa washiriki wa kikao hicho, hawapo kwenye picha.
Prof.Adolf F Mkenda Naibu Katibu Mkuu Wizara ya fedha akitoa mada kwa washiriki wa mkutano huo, hawapo kwenye picha.
Naibu
Waziri wa Fedha ,Mhe. Saada Salum Mkuya akifungua mkutano wa kikao
kazi unaofanyika hapa mjini Bagamoyo kwa muda wa siku mbili. Kikao kazi
hicho kitakuwa na jukumu kubwa la kujadili ripoti ya kutathmini
utendaji kazi wa mfumo wa usimamizi wa fedha za umma ambayo
imeshakamilika( PEFA Report). Lengo kubwa la kikao hicho ni kutafuta
ufumbuzi wa matatizo ambayo yamebainishwa katika ripoti hiyo. Kikao
hicho kitawashirikisha washirika wa maendeleo pamoja Wizara ya fedha
yenyewe.
Naibu
Waziri wa Fedha ,Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa katika picha ya pamoja
na wawakilishi kutoka Serikali ya Tanzania pamoja na Washirika wa
maendeleo kutoka nchi Wahisani.


No comments:
Post a Comment