
Wananchi wa Simiyu wakiwa kwenye mkutano wa pamoja kujadili suluhisho la mauaji ya kikatili eneo lao
Wiki iliyopita katika ukurasa huu, tuliwaletea mwendelezo wa ripoti maalumu kuhusu mauaji yaliyokuwa yakitekelezwa mkoani Simiyu kupitia Baraza la Kimila maarufu Dagashida na jinsi wananchi wanavyoogopa kutoa ushirikiano kwa polisi.
Leo tunaendelea na sehemu ya tatu na ya mwisho ya
ripoti hiyo, pamoja na mambo mengine ikiainisha takwimu za vifo
zilizotolewa na Jeshi la Polisi kutokana na matukio mbalimbali ya mauaji
ya Dagashida.
Wanakijiji hawatoi ushirikiano
Kamanda Msangi anakiri kuwepo kwa changamoto ya kukosa ushirikiano kutoka kwa wananchi wakihofia usalama wao.
“Sisi tunawaomba wasiogope kutoa taarifa za
ukatili huo, lakini pia tunaomba mashirika na dini waendelee
kuelimisha,”anasema Kamanda Msangi.
Anaeleza kusikitishwa kwake na viongozi wa kisiasa
kutoshiriki katika harakati za kukemea ukatili wa baraza hilo
akifafanua tangu alipoanza kazi mkoani Simiyu hajawahi kuona wala
kusikia mbunge yeyote wa mkoa huo akikemea ukatili wa Dagashida.
“Hakuna mbunge au diwani yeyote mwenye nguvu ya
kuzuia baraza hilo kwa sababu wanalitumia kisiasa, kwa hivyo niwaombe
waache kuchanganya siasa na maisha ya watu. Ni vyema wakashiriki
kuelimisha,” anasema.
Polisi na takwimu za mauaji ya Dagashida
Takwimu za Jeshi la Polisi mkoani Simiyu
zinaonyesha kuwa matukio ya mauaji hayo yanahusisha sababu mbalimbali
ikiwamo kugombania mirathi, mipaka ya ardhi, imani za kishirikina pamoja
na kujichukulia sheria mkononi.
Wiki iliyopita Mkuu wa Polisi Mkoa wa Simiyu
Kamishna Msaidizi Salum Msangi alisema: “Nilipoingia Simiyu hali ilikuwa
mbaya sana. Tulipokea ripoti za matukio kama hayo, hata ya watu watano
kuuawa kwa siku, kuona hivyo kwa kushirikiana na mkuu wa mkoa
tulizunguka Mkoa wa Simiyu wote kupiga marufuku uwepo wa baraza hilo…,”
Maelezo hayo ya Kamanda Msangi yalimaanisha kuwa
katika kila siku saba za wiki watu 35 waliuawa mkoani Simiyu na katika
mwezi mmoja wastani wa watu 150 waliuawa katika matukio yaliyohusisha
kikundi cha Dagashida.
Hata hivyo, takwimu za jeshi hilo zilizotolewa
wiki hii zinabainisha kwamba jumla ya watu 117 ameuawa katika vijiji
mbalimbali vya Mkoa wa Simiyu kati ya Juni 2012 hadi Juni 2013.na gazeti la mwananchi
No comments:
Post a Comment