Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, September 8, 2013

Obama aomba kuungwa mkono kuhusu Syria

obama-makes-victory-speech-data_b62fb.jpg
Rais wa Marekani Barack Obama amewahimiza wamarekani kuunga mkono mpango wake kuishambulia Syria huku shinikizo la kidiplomasia likizidi dhidi ya serikali yake kuitaka isubiri ripoti ya wataalamu wa silaha wa umoja wa Mataifa kuhusu mashambulizi hayo ya silaha nchini Syria.

Ripoti hiyo inatarajiwa kutolewa katika kipindi cha wiki moja ijayo.Mawaziri wa mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya waliokutana jana nchini Lithuania wameushutumu utawala wa Rais Bashar al Assad kutumia silaha za sumu dhidi ya raia lakini hawakuidhinisha hatua za kijeshi dhidi yake. Mawaziri hao walitamka wazi kuwa wangetaka umoja wa Mataifa kuwa mstari wa mbele katika maamuzi ya hatua gani jamii ya kimataifa ichukue kuhusiana na uhalifu huo. Huku hayo ya yakijiri kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis hapo jana aliwaongoza kiasi ya waumini bilioni 1.2 kote duniani kuiombea amani Syria,mashariki ya kati na duniani kwa jumla.

No comments:

Post a Comment