Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, September 8, 2013

Julius Nyerere Alipostaafu Serikali Ilimpa Gari Hili Atumie...

macho_ya_panzi_39351.jpg

Ndugu zangu,
Ni gari hii ambalo enzi hizo mitaani ikijulikana kama ' Macho ya panzi'. Mwalimu hakuwa na makuu. Hili ndilo gari alilotumia muda wote baada ya kustaafu.
Na ndilo lililompeleka Airport kwenye safari yake ya mwisho kwenda matibabuni Uingereza. Mwalimu hakurudi tena kuja kulipanda gari hili kumrudisha nyumbani kwake Msasani.
Baadae lilitumiwa na Mama Maria Nyerere, kisha nae, akalikabidhi kwa hiyari yake Makumbusho ya Taifa.
Liko pale Makumbusho ya Taifa Mtaa wa Shaaban Robert. Nayo ni historia yetu.
Jumapili Njema.
na Maggid,

No comments:

Post a Comment