Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, September 10, 2013

SERIKALI YAMPONGEZA MZEE GURUMO



11_fb546.jpg
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Bibi. Lilly Beleko kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akimkabidhi Mzee Muhidini Gurumo barua kama ishara ya Serikali kutambua mchango wake uliotukuka katika tasnia ya Muziki nchini pamoja na kumpongeza kwa kustaafu kazi kazi hiyo, hivi karibuni nyumbani kwake Makuburi, Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia nyuma ya Mkurugenzi ni Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Bw. Addo Mwasongwe na kulia pembeni ya Mzee Gurumo ni Mkewe, Bibi. Pili Said Kitwana.
22_c71f0.jpg
Nguli wa Muziki wa Dansi, Mzee Muhudini Gurumo (aliyevaa shati la drafti) akiwa na watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, walipomtembelea nyumbani kwake Makuburi Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Serikali kupitia Wizara hiyo ilimkabidhi barua rasmi Mzee huyo kutambua mchango wake katika tasnia ya Muziki na kumpongeza kwa kustaafu kazi hiyo. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Bibi Lilly Beleko, wa pili ni mke wa Mzee Gurumo, Bibi. Pili Said Kitwana na wa Pili Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara Upande wa Sanaa, Bibi. Joyce Hagu.
Picha zote na Concilia Niyibitanga

No comments:

Post a Comment