Hatimaye
yule mbaya wa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel aitwaye
Yvonne Maximilian (22) amenaswa na kuhenyeshwa kortini kisa kikiwa ni
kumpiga chupa mwigizaji huyo.Yvonne aliburuzwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Dar baada ya kukamatwa maeneo ya nyumbani kwake
Kinondoni-Manyanya.
Habari za ndani kutoka kortini
zilieleza kuwa awali kesi hiyo ilikuwa isikilizwe na hakimu Agustino
Mbando lakini baadaye kulitokea mabadiliko ambapo ilisomwa na Fundi
Fimbo.
Akiwa mahakamani hapo huku Aunt naye akihudhuria kama mlalamikaji, Yvonne alishuhudiwa akipelekwa puta na polisi.
Hata hivyo, baada ya kesi hiyo kusomwa iliahirishwa hadi Oktoba 17, mwaka huu, itakaposikilizwa tena.
Agosti 26, mwaka huu, Yvonne anadaiwa kumjeruhi Aunt kwa chupa tupu
ya bia na kumpasua mkono wa kushoto wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bilicanas,
Posta jijini Dar.
No comments:
Post a Comment