Mkurugenzi
wa elimu kwa mlipa kodi Taifa Bw Richard Kayombo katikati akizungumza
na wanahabari leo,kulia ni meneja wa TRA mkoa wa Iringa
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
wamekutana na wanahabari mkoa wa Iringa na kueleza mafanikio makubwa
ambayo yamepatikana kutokana na utaratibu mpya wa ukusanyaji mapato
kupitia mitandao ya kama M-Pesa , Tigo Pesa , Airtel Money .Mkurugenzi wa elimu kwa walipa kodi nchini Bw Richard Kayombo ameyase ma hayo mapema leo katika ukumbi wa Hotel ya M.R mjini hapa wakati akizungumza na wanahabari kuhusu utaratibu mpya wa ulipaji wa kodi.(P.T)
Kayombo amesema kuwa kwa mwaka jana
kwa muda wa wiki nne walipata kukusanya kiasi cha Tsh bilioni 3.6 wakati
kwa mwaka huu kwa kipindi cha wiki nne wamepata kukusanya kiasi cha Tsh
bilioni 4.7 ikiwa ni ongezeko la Tsh bilioni 1.1
Hata hivyo Kayombo alisema kuwa TRA imetoa muda hadi Novemba 15 mwaka huu kwa wafanyabiashara kununua mashine hizo kutolea risiti .
Alisema kuwa mashine hizo za utoaji risiti si tu zitasaidia serikali katika kukusanya mapato ila bado zitamsaidia mfanyabiashara kutunza kumbukumbu zake na kuepuka kuibiwa na wafanyakazi wake wasio waaminifu.
Hivyo alisema baada ya kupita Novemba 15 mwaka huu TRA itafanya msako mkali kwa wale wote watakaoshindwa kununua mashine hizo na wale ambao wamenunua mashine hizo na kushindwa kuzitumia.
Kwa alisema kuwa TRA kwa imejipanga kwa miaka mitano ijayo kuwa na huduma endelevu za uboreshaji wa utendaji wake kwenye maeneo matatu .
Eneo la kwanza ni katika ulipaji kodi,walipa kodi kulipa kwa wakati,kuhamasisha ununuzi wa mashine za utoaji risiti.
Pia alisema kuwa lengo la TRA ni kuendelea kuboresha ulipaji kodi na kuwa lazima wafanyabiashara kutambua kuwa suala la ulipaji kodi ni wajibu na sio adhabu kwani hata katika vitabu vitakatifu vinaeleza wazi juu ya wajibu wa ulipaji kodi.
WAFANYABIASHARA KUJITNGAZA
Hivyo alisema kuwa mfanyabiashara ana wajibu wa kulalamika pale ambapo anaona kuwa anakadiliwa isivyo na kuwa TRA haiongezi kodi kwa wafanyabiashara wanaojitangaza katika vyombo vya habari .
Hivyo aliwataka wafanyabiashara kuendelea kujitangaza katika vyombo vya habari ili kupata mafanikio katika biashara zao na kuweza kulipa kodi kulingana na makadilio ya biashara na sio kwa kujitangaza .
" Tunawataka wafanyabiashara kutumia vyombo mbali mbali vya habari kutangaza biashara zao ili kuongeza idadi ya wateja na kuwa TRA hakitozi kodi kutokana na matangazo ....nawaombeni wanahabari msaidie kuwaondoa wasiwasi wafanyabiashara juu ya dhana hiyo potofu kuwa wakijitangaza watafuatwa na TRA ili kuongezewa kodi"
Chanzo:http://www.matukiodaima.com/

No comments:
Post a Comment