Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, October 9, 2013

AFYA LEO::MAFUTA YA KITUNGUU SWAUMU NA MATUMIZI YAKE


HUKO nyuma tumewahi kuelezea kitunguu swaumu na tiba yake, kimekuwa kikitibu magonjwa mengi sana ikiwa ni pamoja na kushusha presha, kupunguza mafuta mwilini, kutibu ugonjwa wa saratani ‘cancer’, magonjwa ya moyo, hutibu pia kuondoa chunusi.
Leo nitakuletea mafuta ya kitunguu hiki ni tiba sana ingawa si watu wengi wanayafahamu, yanapatikana maduka yote ya asili iwapo utayahitaji na kama utakuwa hukunielewa hapa unaweza kupata matumizi yake sahihi pale utakapokwenda kuyanunua kwa wataalamu wanaoyauza.
Mafuta haya ukiyatumia ipasavyo yanao uwezo wa kutibu ugonjwa wa mafua, kikohozi kilichoshindikana, yanauwezo wa kutibu fangasi za aina yote na magonjwa mengine mengi.
Kwa wanaopunguza mafuta mwilini
Asubuhi unachukua glasi yako ya maji ya kunywa ambayo umeshayachemsha, yakiwa na uvuguvugu tayari kwa kunywa weka kijiko kimoja kikubwa cha kitunguu swaumu kunywa kila siku asubuhi. Kila mara jaribu kupima uzito utaona matokeo kwani ni tiba nzuri sana mbali na kupunguza mafuta yasiyohitajika mwilini pia yana uwezo wa kupunguza uzito kwa kiasi chake.
Kwa mtu aliyebanwa na mafua
Chukua kitambaa kisafi loweka kwenye mafuta kiasi ni mafuta yenye harufu kali ambayo unaweza usiivumilie lakini kitiba yanatibu kwa haraka sana.
Kama una uwezo wa kuweka kwenye maji yaliyochemka na kujifukiza, husaidia kufungua pua na kukutibu kikohozi ambacho huletwa na mafua.
Kwa akina mama wanaotaka kurudisha umwari wao
Kwa wale akina mama ambao wamekuwa na tabia ya kutaka kurudisha umwari wao, hasa wale waliozaa na wale ambao wanahisi hawako sawa mafuta haya yanasaidia iwapo utapaka hasa wakati wa kulala.
Kwa kutibu fangasi
Fangasi wapo wa aina nyingi hapa niongelee wa miguuni na wa sehemu za siri.
Mafuta haya yanatibu kwa asilimia kubwa tatizo la fangasi kama unao wa miguuni, chukua mafuta haya yapashe kidogo yaache yapoe, osha miguu yako ikaushe mpaka katikati ya vidole kisha chukua mafuta ya kitunguu swaumu paka mpaka utakapoona umepona.
Kwa walio na fangasi wa sehemu za siri hasa akina mama, chukua maji ya vuguvugu, weka mafuta hayo kiasi cha vijiko viwili kwenye maji nawa na maji hayo sehemu za siri unaweza kufanya hivyo mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni
Maumivu ya sikio
Kama unasumbuliwa na sikio mafuta haya ni tiba nzuri, chukua mafuta yapashe yaache yapoe kabisa, kisha dondoshea tone moja kwa mtoto na kwa wakubwa matone 2-3, kama huna mafuta haya unaweza kuchukua mafuta ya mzaituni ukayapasha kidogo nayo uache yapoe kisha changanya na vipande viwili vya vitunguu swaumu udondoshee kama mafuta hayo, fanya hivyo mpaka utakapopona
Kumbuka
Mafuta ya kitunguu swaumu ni makali kidogo kwa wale wenye ngozi ambayo haiendani, unashauriwa kuchukua tahadhari. Ukiona hayakufai unashauriwa kuacha mara moja.
Kumbuka kwenda hospitali kabla ya kutumia tiba hizi ili kugundua tatizo ulilonalo, kuna watu wengine wanapenda kutumia tiba hizi kwa kusoma hapa tu kila mgonjwa anashauriwa kufika hospitali na kubaini tatizo alilonalo.
Hapa ni msaada tu, kama unahisi una tatizo kubwa waone watabibu wa tatizo hilo na tiba nilizoelezea zitakusaidia.

No comments:

Post a Comment