Gari la mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero likiwa nje ya kituo cha polisi Dakawa..
Vurugu
za wakulima zimezuka tena Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ,ambapo
kundi la wakulima limefunga barabra ya Turiaani-Morogoro eneo la Mkindo
wakipinga wafungaji kuchoma nyumba kadhaa za wakulima sambamba na
kushinikiza serikali kuwaruhusu kulima kwenye bonde la Mgongolwa.Katika
vurugu hizo wakulima hao walirusha mawawe yaliyosababisha Polisi mmoja
kukimbizwa hospital baada ya kupigwa jiwe kwenye paji la uso huku gari
la mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero likihalibika vibaya
baada kupigwa mawe na wakulima hao.
Askari wa jeshi la Polisi akikagua gari la mkurugenzi lililoaribiwa vibaya katika vurugu hizo.
waandishi
wa habari wa waliofika eneo la tukio pia walipigwa mawe na wakulima hao
na kushindwa kutekeleza majukumu yao na kuamu kuondoka eneo hilo la
tukio.Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Bw Anthony Mtaka alilaani kitendo
kilichofanywa na wakulima hao na kulipongeza jeshi la polisi kwa kutumia
hekima kwenye vulugu hizo licha ya kupigwa mawe na wakulima hao
Kundi la polisi wa kutuliza ghasi kutoka moorogoro mjini likieleka eneo la tukio
No comments:
Post a Comment