Ufoo Saro akiwa kitandani hospitalini. |
Mwandishi wa habari wa kituo cha
televisheni cha ITV, Ufoo Saro, aliyejeruhiwa kwa risasi juzi na kulazwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi, kwa sasa hali
yake inazidi kuimarika.
Akizungumza na mwandishi jana, Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo,Aminieli Aligaeshaalisema hali ya mwandishi huyo inazidi kuimarika, lakini bado anatakiwa kuendelea kupumzika zaidi.
“Ufoo,
hali yake kwa sasa ni nzuri, anazungumza na anatambua watu lakini kwa
sasa haturuhusu watu kumtembelea isipokuwa ndugu zake tu kwa sababu
anatakiwa kupumzika zaidi… nafikiri ataruhusiwa watu kumtembelea baada
ya siku mbili au tatu kuanzia sasa,” alisema.
Ufoo
alijeruhiwa kwa risasi Jumapili asubuhi na mzazi mwenzie, Anthery
Mushi, nyumbani kwa mama yake, Anastazia Saro aliyepigwa pia risasi na
kufa papo hapo. Pia mwanaume huyo alijiua.
Baada
ya tukio hilo, Ufoo alipelekwa katika hospitali ya Tumbi iliyopo
Kibaha, ambapo baadae alihamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili
na kufanyiwa upasuaji, ambapo kwa sasa anaendelea vyema.
No comments:
Post a Comment