Jengo la TTCL lenye ghorofa 12 lililoshika moto katika ghorofa ya sita.
Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kutoka Halmashauri ya jijini likifika katikam eneo la tukio.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto wakijiandaa kukabiliana na moto huo.
Askari
wa Kikosi cha Zimamoto akijiandaa kuingia ndani ya ofisi za TTCL
zilizoshika moto, hata hivyo kutokana na kuwa na vifaa duni walishindwa
kuingia ndani.
DAR ES SALAAM, Tanzania
Jengo la TTCL, Makao makuu, EXTELECOMS limeungua moto kuanzia majira ya leo saa 12:00 asubuhi hadi saa 1:20.
Moto huo ulikuwa unawake katika ghorofa ya sita ya jengo hilo na ulikuwa unawake katika vyumba vitatu kwa mara moja.
Habari
Mseto ilifanikiwa kufika mapema katika jengo hilo na kukuta pilika
nyingi za wafanyakazi kuondoa magari yao, na magari ya shirika hilo
kongwe nchini.
Magari ya
kikosi cha zimamamoto kutoka kikosi cha ukoaji cha Jiji la Dar es
Salaam yaliwasili saa 12:20, lakini kulikuwa na ubishani kati ya
wafanyakazi wa zima moto na wale wa TTCL, baada ya wafanyakazi wa
Zimamoto kulaumu kuwa walienda pale siku kadhaa zilizopita kukagua jengo
lakini walifukuzwa kama mbwa,
Licha ya
Kikosi hicho kuwahi hawakuwa na maji yenye pressure na ngazi za nje
kufika hadi ghorofani, hali iliyopelekea watu kutumia ngazi za ndani
kuingia kwenye jengo hilo hali ambayo ni hatari kwa maisha yao.
Gari ya Ultimate Security walifika mnamo saa 12:30 na kwa ushirikiano moto uliweza kufanikiwa kuzimwa.
CHANZO: HABARI MSETO
CHANZO: HABARI MSETO
No comments:
Post a Comment