Mmoja
wa wakazi wa mtaa huu aliye amua kujitoa na kushika kinyesi ili apate
kuzibua chemba ambayo ilikuwa inamwaga maji bila kusimama kwa siku Sita
Hali hii ilikuwa mbaya jambo ambalo wananchi waliamua kujitolea na kufanya wawezalo ili kuzibua
Hali
ni Tete eneo Hili ambapo sasa moja ya Chemba inazidi mwaga maji.. hapa kila mtu
anatoa wazo lake nini kifanyike ili kuweza kuzibua eneo hilo ambalo
maji yake yalikuwa hayapungui kumwagika bali kuongezeka..na mwisho wote waliona bora washike kinyesi kuliko kuendelea kuteseka.
Ilikuwa
ni Baada ya Kuhangaika sana wakazi wa eneo hili kwa kutumia nyenzo yao Duni
ya nondo maalumu ya kuzibulia chemba waliyo jinunulia wenyewe , hatimaye
walifanikiwa kuzibua chemba moja na kuhamia chemba ya pili .
Baada ya Chemba ya Juu kuzibuka , kasheshe ikahamia katika chemba ya pili ambapo sasa maji yote yalihamia hapo.
Masikini mtazame Mama huyu alivyo Ruka juu na mtoto akiwa amemshika kihatari namna hii... hii ni adha ya haya maji taka.
Wakazi wa eneo hili wakiwa wanakomaa kwa nguvu zote kuanza kuzibua chemba ya pili.
Zoezi
sasa linaendelea na hapa walikuwa wanaendelea kuzibua chemba ya 3
ambapo sasa walifika kikomo baada ya kuonekana chemba hiyo ilikuwa
imejaa matakataka ya kutosha pamoja na Mchanga . Na ndipo walipo pata taarifa kuwa DAWASCO
wanakuja.
Wakiwa wamefika kabisa na kujionea Adha ya kukanyaga maji Taka ...... huo nyuma ni mtambo maalum wa kuzibua Chemba
Wafanyakazi
wa DAWASCO wakiwa wamefika katika eneo la tatizo na kuanza kuzibua
chemba za maji taka ili kuwasaidia wakazi hao wasipatwe na magonjwa , Kero
ya maji mtaani na Harufu mbaya
Wakiwa wanahakikisha kabisa kwamba tatizo limekwisha eneo hilo...
Moja
ya Chemba ambayo wakazi wa Mwenge walikuwa wamehangaika nayo sana mpaka kufanikiwa
kutoa maji taka hayo yaende ikiwa inaangaliwa na wafanyakazi wa DAWASCO
Wafanyakazi wa DAWASCO wakiwa wanaendelea kutoa takataka katika chemba sugu ili kuruhusu maji yapite
Hii ni Baada ya Chemba Kuzibuliwa na wananchi wakishirikiana na DAWASCO Ambao walichelewa kufika eneo la tukio
Maji yakionekana yanaendelea kukauka baada ya Chemba hizo kuzibuliwa
Hizi ni Takataka zilizo bakia baada ya kuzibua Chemba hizo ...
Wananchi mtaa wa mwenge
waandamana na kufanya usafi kufuatiwa na kero kubwa ilyokuwa sugu na
hatari katika afya zao, kero hiyo ikiwa ni kuziba na kufumuka kwa chemba zinazo pitisha maji machafu
maarufu kama (majitaka )
Ikiwa nizaidi ya wiki mbili wakazi na watumiaji wa njia ya mwenge
katika mtaa huo uliogeuzwa jina na kupewa jina mahususi na mazingira ya mtaa
ambalo ni mtaa wa( kinyesi street) wamekumbwa na kero ya kufumuka kwa chemba za
maji taka na kuwa na harufu mbaya hivyo wananchi wamehofia afya zao nakuanza
kuzibua Chemba za maji hayo huku kila baada ya mwezi huletewa Bili na kuweza kuzilipia bila ya wasiwasi
.Lakini kibao kimegeuziwa kwa wananchi kuwa ndio wamiliki wa shirika la maji
safi na taka (DAWASCO) leo hii waamua kuondoa adha hiyo iliyo dumu kwa muda
mrefu bila ya ufumbuzi kwa kushika Kinyesi na maji machafu kutoka sehemu
mbalimbali.
Hata hivyo wakazi walilalamika kuhusu
utendaji kazi wa dawasco kuwa ni mbovu kwa kuwa wame watafuta zaidi ya
mara kadhaa bila mafanikio
Aidha wananchi walionekana kuwa na moyo mmoja wa ushirikiano
kufuatia harufu mbaya iliyokuwa ikitoka katika chemba hizo nakufanikisha
kuzibua chemba zote katika mazingira magumu yanayo weza kusababisha maradhi
mbalimbali kwa jamii husika wameongeza kuwa wana iomba mamlaka ya maji
(DAWASCO) hususani kitengo cha majitaka kuweza kupita kila baada ya wiki moja
ili kuweka mazingira mazuri/safi.
No comments:
Post a Comment