Rais
Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Vyama vya upinzani
na wasaidizi wao waandamizi muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu
rasimu ya katika ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto mbele
Isaack Cheyo UDP, James Mbatia NCCR Mageuzi, Professa Ibrahim Lipumba
CUF, Freeman Mbowe CHADEMA, Philip Mangula CCM, na Bibi Nancy Mrikaria
aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mhe.Agustine Lyatonga
Mrema.Waliosimama Nyuma kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu CUF Bwana
Julius Mtatiro,Mhe. Tundu Lissu CHADEMA, Bwana Martin Mng’ong’o NCCR
Mageuzi ,Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge
William Lukuvi, Mhe.Habib Mnyaa CUF, Mbunge wa Ubungo Kwa tiketi ya
CHADEMA Mhe.John Mnyika, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na
Uratibu Mhe.Steven Wassira na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Mathias
Chikawe. (picha zote: Freddy Maro/IKULU).
TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KURUGENZI YA MAWASILIANO IKULU
MKUTANO kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa vyama vya
siasa vyenye uwakilishi Bungeni umemalizika Ikulu, Dar Es Salaam, muda
mfupi uliopita leo, Jumanne, Oktoba 15, 2013 kwa pande hizo mbili
kukubaliana kama ifuatavyo:
Moja , kwamba vyama vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Sheria ya Kurekebisha
Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba viwasilishe mapendekezo yao haraka Serikalini
ili ifatutwe namna ya kuyashirikisha mapendekezo hayo katika marekebisho
ya Sheria hiyo.
Pili, kwamba vyama vya siasa nchini, kama
wadau muhimu katika mchakato wa Katiba Mpya, viangalie namna ya kukutana
na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano wa jinsi kwa pamoja
vitakavyosukuma mbele mchakato huo kwa maslahi mapana ya nchi yao na
mustakabali wa taifa. Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimepewa
jukumu la kuratibu jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa
vyama hivyo na wadau wengine nchini.
Viongozi wa vyama vyama vya siasa
waliokutana na Mheshimiwa Rais Kikwete ni Mheshimiwa Profesa Ibrahim
Lipumba, Mwenyekiti wa CUF; Mheshimiwa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa
CHADEMA na Mheshimiwa James Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.
Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM
Mheshimiwa Philip Mangula, Mheshimiwa Isaack Cheyo ambaye amemwakilisha
Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mheshimiwa John Cheyo na Mheshimiwa Nancy
Mrikaria ambaye amemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mheshimiwa Augustine
Mrema. Waheshimiwa John Cheyo na Mrema wako nje ya nchi.
Wengine ambao wameambatana na
wenyeviti wao ni Mheshimiwa H. Mnyaa na Bwana Julius Mtatiro wa CUF,
Waheshimiwa Tundu Lissu na John Mnyika wa CHADEMA na Bwana Martin
Mng’ongo wa NCCR-Mageuzi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
15 Oktoba, 2013
No comments:
Post a Comment