Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, October 30, 2013

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA POLISI KWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU NA UFUNDI...


Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili wahitimu walioorodheshwa hapa chini wa vyuo vya Elimu ya Juu na  vya Ufundi  Stadi.
Usaili utafanyika kuanzia tarehe 11/11/2003 hadi tarehe 15/11/2013 saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni kila siku kwa taaluma na maeneo yafuatayo;
  •  Fani za Menejimenti  ya Rasilimali Watu, Utawala, Uchumi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji(BaLe), Ualimu, Sosholojia, Saikolojia na Ushauri Nasihi, Sheria, Takwimu, Lugha, Uhusiano wa Kimataifa, Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma, Maendeleo ya Jamii, Ukutubi na Utunzaji Kumbukumbu. Usaili  wa fani hizi  utafanyika katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam(DPA) kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam .
  • Fani ya Udereva ,Ufundi rangi za magari(spray and Painting /Panel Beating ), Ufundi wa matengenezo ya Magari Makubwa(Auto-Mechanics-Heavy Duty) na Ufundi wa Matengenezo ya Umeme wa Magari(Auto Elecrical ). Usaili wa  fani hizi utafanyika Kikosi cha Polisi Ufundi kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
  • Fani za Kompyuta. Usaili wao utafanyika nyuma ya kikosi cha Ufundi yaani  TEHAMA KEKO chini.
  • Fani ya Uhandisi Mitambo(Mechanical Engineering ). Usaili wao utafanyika Kikosi cha Polisi Anga kilichopo Uwanja wa Ndege JK Nyerere DSM.
  • Waataalam wa masuala ya Afya/Wauguzi usaili wao utafanyika katika kikosi cha afya kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
  • Orodha  ya majina inapatikana  pia katika Gazeti la habari Leo la tarehe  04/11/2013.
   Muhimu: 
  1. (i)Mwombaji afike kwenyeakiwa na nakala  halisi  pamoja na kivuli cha  vyeti vyote vya masomo/Taaluma [Academic Transcript (s)/Certificate(s)]yaani  kidato cha nne, sita ,Chuo na cheti cha kuzaliwa. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika. 
  1. (ii)Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atalipia gharamaupimaji afya  shilingi elfu kumi(10,000), usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili.
 (iii)Kwa kuwa  muda ni mchache  anaekuja kwa usaili ajiandae baada ya usaili atakaechaguliwa  atapelekwa katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi siku nne baada ya usaili kwisha yaani tarehe 19/11/2013.
 Orodha ni kama ifuatavyo;

BOFYA HAPO CHINI UDOWNLOAD MAJINA

SOURCE: http://www.policeforce.go.tz

No comments:

Post a Comment