skip to main |
skip to sidebar
TASWIRA ZA KUANZA KWA WIKI YA VIJANA MKOANI + KITAIFA IRINGA
Viunga vya mji wa Iringa, Mkoa wa
Iringa ni Mwenyeji wa Wa Wiki ya Vijana Kitaifa, kumbukumbu ya Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka
2013.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto wakitoa
elimu kwa baadhi ya wakazi wa Iringa namna kutumia vifaa vya kuzimia
moto na jinsi ya kukabiliana na majanga ya moto katika maeneo yao leo
wakati wa maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani
Iringa.
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa
waliofika katika banda la maonyesho la VETA Iringa wakipata maelezo ya
bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na na VETA kutoka kwa Bi. Oliva
Adriano mwanafunzi wa mwaka wa 3 katika chuo cha Ufundi (VETA) mkoa wa
Iringa.
Vijana wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA)
mkoa wa Iringa wakionyesha ujenzi wa nyumba za gharama nafuu wakati wa
Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa mkoani Iringa leo.
Baadhi ya Watoto wakiangalia banda la
Vijana kutoka mkoa wa Dar es salaam na bidhaa mbalimbali
zilizotengenezwa na Vijana hao leo katika viwanja vya Mlandege mkoani
Iringa.
Picha na Aron Msigwa -MAELEZO
No comments:
Post a Comment