Huyu
ndiye marehemu kijana maarufu kwa jina la 'Mkandarasi' anayesadikika
kufanya mauaji kwa mumchoma kijana mwenzake kisu naye aliuawa na
wananchi wenye hasira katika mtaa wa Msikiti wa Ijumaa jijini Mwanza.
Umati wa watu mtaa wa Msikiti wa Ijumaa.
Mashuhuda wakiutizama mwili wa kijana aliyeuwa kwa kuchomwa kisu.
Mwili wa kijana aliyekuwa akifanya kazi kwa mamalishe mtaa wa Msikiti
wa Ijumaa ukiwa umelowa damu mara baada ya kuchomwa kisu kufuatia
majibizano na jamaa (maarufu kwa jina la 'Mkandarasi') ambaye naye
aliuawa na wananchi wenye hasira waliojichukulia sheria mkononi.
Mashuhuda.
Polisi walifika eneo la tukio na kisha wakaondoka na miili ya
marehemu hao nao wengine wakibakia eneo la tukio kubaini nini chanzo.
Mwananchi akifukia damu zilizotapakaa kwenye barabara.
Watu
wawili wameuawa katika tukio la utata lililotokea jana asubuhi majira
ya saa 3 na dakika kadhaa, katika eneo la barabara ya msikiti wa Ijumaa
jijini Mwanza.
Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa kilisababishwa na kijana mmoja
maarufu kwa jina la Mkandarasi kumchoma kisu kijana mwenzake ambaye
alikuwa mgeni akifanya kazi za usaidizi kwa mamantilie wanaopika chakula
katika moja ya viunga vya ndani eneo la vichochoro vya mtaa wa Msikiti
wa Ijumaa kufuatia majibizano ambayo yalisababisha kijana Maarufu kwa
jina la 'Mkandarasi' amchome mwenzake kisu cha shingoni na sehemu
nyingine za mwili.
Kijana huyo alipoona amezidiwa alitafuta upenyo na kukimbia huku damu
zikimchirizika, hata hivyo hakufika mbali kwani alizidiwa na hatua
chache baadaye alianguka chini nakuaga dunia.
Wananchi wenye hasira walimzingira muuaji ambaye naye alikuwa
akijihami kwa kisu alichokuwa nacho mkononi na ndipo walipofanikiwa
kumbwaga chini na kumshambulia kwa mawe hadi umauti.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linataraji kuja na taarifa kamili ya Uchunguzi wake hii leo.
No comments:
Post a Comment