Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kimewaandikia barua za kuwavua rasmi nyadhifa za uongozi aliyekuwa naibu katibu mkuu Mh. Zitto Kabwe na wenzie sambamba na kupewa siku kumi na nne za kujieleza kwa nini wasivuliwe uanachama kufuatia waraka wa siri walioundika na kukamatwa hivi karibuni.
Mkurugenzi wa habari na uenezi Chadema Mh. John
Mnyika amesema barua hizo zilizoainisha makosa kumi na moja ya kukiuka
katiba na itifaki za chama hicho zitawataka wahusika kujieleze kwa
maandishi na baadae mbele ya chama kwa nini wasifukuzwe na kuvuliwa
uwanachama kufuatia waraka waliouandaa uliosemekana ulilenga kikupindua
chama hicho.
Aidha Mh. Mnyika ameongeza kuwa waraka uliochapisha
kwenye baadhi ya magazeti na mitandao mbalimbali ya kijamii sio ule
uliowahukumu wahusika hao na kuwaomba watanzania na wafuasi wa chama
hicho kutoutilia maanani waraka huo na siku itakapobidi kuutoa waraka
husika watafanya hivyo.
Awali mwanasheria mkuu wa chama hicho Mh. Tundu
Lissu akizungumzia mkutano uliofanywa na Mh. Zitto na wenzie licha ya
kukata kusema hatua zitazozochukuliwa pindi watakaposhindwa kutimiza
mashati waliyoyaweka amesema mkutano huo ulilenga kupoteza lengo kuu la
kuvuliwa madaraka na kuwa kilichowafukuza ni mkakati wao wa siri
uliolenga kukipindua chama hicho na si vinginevyo.CHANZO ITV
No comments:
Post a Comment