
TIMU ya taifa
ya Ghana, imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la
Dunia mwakani nchini Brazil, licha ya kufungwa mabao 2-1 na Misri katika
mchezo uliomalizika muda mfupi uliopita kwenye Uwanja wa jeshi mjini
Cairo.
Ghana imefuzu kwa ushindi wa jumla ya mabao 7-3, baada ya kufanya
kazi nzuri katika mchezo wa kwanza mjini Kumasi mwezi uliopita na sasa
watakwenda Brazil kujaribu kuendeleza mafanikio ya fainali zilizopita
Afrika Kusini mwaka 2010 walipofika Robo Fainali.


Misri,
waliokuwa wakicheza nyumbani kwa mara ya kwanza mjini Cairo ndani ya
miaka miwili, walianza vizuri na kuongoza kwa 2-0, mabao ya mshambuliaji
wa Wigan Athletic, Amr Zaki na Gedo.
Lakini Kevin-Prince Boateng akaifungia Ghana bao la kufutia machozi
dakika za lala salama na kufanya matokeo yawe 7-3, baada ya awali
kushinda 6-1 nyumbani.
Ghana imeungana na timu nyingine tatu za Afrika kufuzu kwenye fainali
hizo, Ivory Coast, Nigeria na Cameroon na mchezo kati ya wenyeji
Algeria na wageni Burkina Fasso utakamilisha idadi
ya timu tano zitakazoliwakilisha bara hili kwenye fainali hizo.
Katika mchezo wa kwanza, Burkina Faso ilishinda 3-2 nyumbani, maana
yake Algeria hata wakishinda 1-0 leo nyumbani kwao, watafuzu pia.


No comments:
Post a Comment