Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji
kilichofanyika leo (Novemba 23 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Rais
Malinzi alisema kamati hizo zimeundwa kwa mujibu wa katiba ili kuisaidia
Kamati ya Utendaji.
Pia
ametangaza wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji aliowateua. Wajumbe hao
ni Richard Sinamtwa na Ramadhan Nassib, wakati wengine wanaoingia moja
kwa moja kwenye Kamati ya Utendaji kutokana na kamati wanazoziongoza ni
Dk. Paul Marealle na Saloum Umande Chama.
Kamati
ya Fedha na Mipango inaongozwa na Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia
wakati wajumbe ni Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Omari Walii,
Eliud Mvella, Said Muhammed, Geofrey Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub
Nyenzi, Lina Kessy na Cyprian Kuhyava.
Geofrey
Nyange anaongoza Kamati ya Mashindano wakati wajumbe ni Clement Sanga
(Makamu Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro,
Moses Katabaro, Seif Ahmed, Gerald ambi, Davis Mosha, Said George na
Nassoro Idrissa.
Kinara
wa Kamati ya Ufundi ni Kidao Wilfred wakati wajumbe ni Athumani Kambi
(Makamu Mwenyekiti), Vedstus Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi,
Patrick Kahemele, Daud Yassin, Nicholas Mihayo na Dk. Cyprian Maro.
Kamati
ya Mpira wa Miguu wa Vijana inaongozwa na Ayoub Nyenzi, Khalid Abdallah
(Makamu Mwenyekiti), Ali Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said
Tully, Luteni Kanali Charles Mbuge, Lameck Nyambaya na Ibrahim Masoud.
Lina
Kessy anaongoza Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake wakati wajumbe ni
Shyrose Bhanji (Makamu Mwenyekiti), Zena Chande, Amima Karuma, Dk.
Cecilia Makafu, Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma,
Martin Mung’ong’o na Engrid Kimaro.
Kamati
ya Waamuzi inaongozwa na Saloum Umande Chama, Nassoro Said (Makamu
Mwenyekiti), Charles Ndagala (Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro
Chacha, Paschal Chiganga, Victor Mwandike, Soud Abdi na Zahra Mohamed.
Hamad
Yahya Juma ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anaongoza Kamati ya
Habari na Masoko wakati wajumbe ni Naibu Waziri January Makamba (Makamu
Mwenyekiti), Tido Mhando, Yusuf Manji, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla,
Jack Gotham, Fredrick Mwakalebela na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi
wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inaongozwa na Richard Sinaitwa, Moses
Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hanspoppe, Hussein Mwamba, Philemon
Ntahilaja, Abdul Sauko na Imani Madega.
Kiongozi
wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha ni Ramadhan Nassib wakati wajumbe ni
Zitto Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Nicholas Magarinza, Jackson Songora,
Epaphra Swai, Kalilo Samson, Goodluck Moshi, Golden Sanga na Elias
Mwanjala.
No comments:
Post a Comment