
Mke wa zamani wa Nelson Mandela, amesema rais huyo wa zamani hawezi kuzungumza, lakini anatumia uso kuwasiliana na watu.
Winnie
Madikizela-Mandela alieleza kuwa Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 95,
ni mgonjwa kweli lakini alikanusha tetesi kuwa mashini ndio inamsaidia
kupumua.
Mwezi wa
Septemba Bwana Mandela alirudi nyumbani baada ya kulazwa hospitali mjini
Pretoria kwa karibu miezi mitatu akitibiwa ugonjwa wa mapafu.
Serikali ya Afrika Kusini imesema hali yake bado ni ya kutia wasi-wasi na wakati mwengine hubadilika.

No comments:
Post a Comment