Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, November 18, 2013

Zanzibar kuanza utafiti wa awali wa uwezekano wa kuwepo mafuta baharini


Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makazi,maji,Nishati na Madini Zanzibar Nd. Ali Khalil Mirza na Mwenzake Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya utafiti na uchimbaji wa Mafuta na Gesi Bwana Kamal Ahaya wakiweka saini mkataba utakaotoa fursa kwa Wataalamu na Wahandisi wa Kampuni ya Ras Gas ya Ras Al –Khaimah kufanya utafiti wa awali wa uwepo wa rasilmali ya mafuta na Gesi Zanzibar.Wanaoshuhudia nyuma yao kutoka kulia ni Mfalme wa Ras Al – Khaimah Sheikh Saud Bin Saqr Al – Qasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddipanoja na Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji Nishati na Madini Mh. Ramadhani Abdulla Shaaban.


Serikali ya Ras Al – Khaimah na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimetiliana saini mkataba utakaotoa fursa kwa Wataalamu na Wahandisi wa Kampuni ya Kimataifa ya utafiti na uchimbaji wa mafuta na Gesi ya Ras Al –Khaimah { Ras Gas } kufanya utafiti wa awali { SCAUT } katika maeneo ya ardhi na Baharini ili kupata uhakika wa uwepo wa rasilmali ya mafuta na Gesi Zanzibar.
Mkataba huo umetiwa saini katika hafla maalum iliyofanyika katika Jumba la Kifahari la Kifalme la Al -Dhait Palace Nchini Ras Al – Khaimah na kushuhudiwa na Mfalme wa Nchi hiyo Sheikh Saud Bin Saqr Al – Qasmi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiuongoza Ujumbe Mzito wa Mawaziri Saba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa Upande wa Zanzibar Saini hiyo imetiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji, Nishati na Madini Nd. Ali Khalil Mirza wakati ule wa Rais Al – Khaimah imewekwa na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya utafiti na uchimbaji wa Mafuta na Gesi ya { Ras Gas } Bwana Kamal Ahaya.

No comments:

Post a Comment