Rais
Mstaafu Benjamin Mkapa akipongezwa na Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo
jana wakati misa ya jubilei ya miaka 75 ya kuzaliwa kwake. Picha na
Fidelis Felix. Dar
es Salaam.Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa jana aliadhimisha miaka 75 ya
kuzaliwa kwake kwa kufanya Ibada ya Misa iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo
Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.Katika
ibada hiyo ya shukrani iliyofanyika Kanisa Katoliki la Maria Imakulata,
Upanga jijini Dar es Salaam, Mkapa aliwataka Watanzania kumshukuru
Mungu kwa kila jambo.“Tunamshukuru
Mungu kwa majaliwa aliyoipatia nchi yetu ya Tanzania na tunamwomba
azidi kuijalia umoja katika yote tunayofanya na tunayokusudia
kuyafanya,” alisema Mkapa.Mkapa
pia aliwashukuru waumini wenzake katika kanisa hilo, huku akifichua
siri kwamba, Kadinali Pengo alimtaka ahamie Kanisa la Mtakatifu Joseph
wakati alipokuwa rais, lakini hakukubali.
Kwa upande wake, Kardinali Pengo aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kumshukuru Mungu kwa kila jambo.
“Alichofanya
Rais Mstaafu Mkapa ni cha kuigwa. Tunatakiwa kutambua kuwa hatuishi kwa
nguvu zetu bali kwa uwezo wa Mungu hivyo ni lazima tumshukuru kama
alivyofanya mwenzetu,” alisema Kardinali Pengo.
Baadhi
ya viongozi waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Mawaziri Wakuu
Wastaafu, Edward Lowassa na Cleopa Msuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi na Mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Wengine
ni waziri wa zamani, Profesa Philemon Sarungi, Askofu Mkuu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa pamoja wakuu wa
zamani wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Majenerali, Robert
Mboma na George Waitara.
No comments:
Post a Comment