Mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne mwaka huu, Sharifa Abdallah (18) ameuawa kwa kuchomwa kisu shingoni na mbavuni chumbani kwa mvulana aliyedai kuwa mpenzi wake maeneo ya Kimara Golani, Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 8:30 mchana na baadaye mvulana huyo aliyetambuliwa na Polisi kwa jina la Abdul Alpha (22) kujisalimisha katika kituo cha Polisi cha Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo, akidai alikuwa akitaka kutoroka lakini aliona amefanya dhambi kubwa.
Akizungumza
na mwandishi jana, mama mkubwa wa marehemu, Mwajuma Khamis alisema
Sharifa alimaliza kidato cha nne katika sekondari ya Luguruni na alikuwa
akisubiri matokeo.
Alisema juzi waliporejea kutoka kazini
hawakumkuta nyumbani, waliulizia kwa ndugu kutokana na kwamba hakuwa na
tabia ya kutoka nyumbani, lakini hawakufanikiwa kumpata hadi jioni ndipo
polisi walipowataarifu kupatikana kwa mwili wake.
Alisema mwili wa
marehemu ulikutwa chumbani kwa kijana huyo karibu na nyumbani kwao ukiwa
na majeraha mwilini, lakini hawakujua kama mtoto wao ana mwanaume,
wanatarajia kumzika kesho saa saba mchana.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema polisi walipata taarifa za tukio
hilo katika kituo cha Ubungo na kwenda katika chumba cha kijana huyo
kilichokuwa kimefungwa kwa ndani na kukuta mwili wa msichana huyo ukiwa
umejeruhiwa.
Alisema baada ya kumhoji mtuhumiwa, alisema alifanya
hivyo kutokana na wivu wa kimapenzi, kwani alikuwa na uhusiano na
msichana huyo lakini wazazi wa msichana hawakutaka amwoe, hivyo
kumtaarifu kuwa amepata mchumba mwingine.
Alipoulizwa kwa nini
hakutoa taarifa katika kituo cha Polisi Kimara alikofanyia mauaji,
alisema aliogopa watu wa maeneo yale wangempiga na kumwua, kwa kitendo
hicho.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Tumbi, Kibaha, huku kijana huyo akishikiliwa na Polisi.
-Zero99
-Zero99
No comments:
Post a Comment