Kiongozi
wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh
Azzan Khalid Hamdan amerejea nchini akitoke India alikokwenda kwa ajili
ya matibabu na kutakiwa kurejea tena Desemba 15, mwaka huu .
Sheikh
Azzan aliaachiwa kwa dhamana ya matibabu akiwa miongoni mwa washtakiwa
kumi waliofunguliwa kesi ya uharibifu wa mali na kuhatarisha Usalama wa
Taifa, kesi ambayo inaendelea Mahakama Kuu visiwani Zanzibar
Akihojiwa
na gazeti hili nyumbani kwake Mfenesini, Mkoa wa Kaskazini Unguja,
Sheikh Azzan alisema baada ya kufanyiwa uchunguzi wa figo, madaktari
bingwa wamemtaka kurejea tena nchini India Desemba 15, mwaka huu kwa
ukaguzi wa mwisho wa afya yake.Sheikh Azzan alirejea nchini Novemba 8,
mwaka huu baada ya kukamilisha matibabu yake katika Hospitali ya Manipal
nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu na baadaye kupumzika Muscat
Oman kwa muda wa wiki kabla ya kurejea Zanzibar.Akitoa tathmini ya
maendeleo ya afya yake, Sheikh Azzan alisema alipofika Hospitali jambo
la kwanza alifanyiwa uchunguzi na kuonekana ana matatizo makubwa matatu
moja likiwa ni kupatikana na mawe 17 katika figo zake zote mbili,
alitibiwa kwa mionzi na kuvurugwa mawe.
“Walinipiga
mionzi katika figo langu la kwanza na kisha wakanipiga la pili na
kuyavuruga mawe yote na kutoka mwilini kwa njia ya mkojo,” alisema
Azzan.
Katika
uchunguzi wa daktari aliofanyiwa, Sheikh Azzan alipatikana akiwa na
tatizo la maumivu ya kichwa ambapo awali alikuwa akilalamika kuwa na
maumivu makali pamoja na kukosa usingizi kwa muda mrefu.
Alisema
daktari alimshauri apunguze matumizi ya simu ya mkononi (mobile phone)
ili kujaribu kutuliza hali hiyo pamoja na kumpa dawa za kupunguza
maumivu kwa muda wa miezi miwili mfululizo.
Akitaja
tatizo la tatu, Sheikh Azzan alisema madaktari waligundua ana michubuko
na vidonda katika tumbo na kutakiwa katika hatua ya awali kujipangia mlo
na kuacha kula baadhi ya vyakula vikiwamo vile vyenye virutubisho vya
Protein kama nyama ya ng’ombe, kuku, samaki, zabibu na maboga.
Alipoulizwa
kama atarejea rumande Sheikh Azzan alisema, hakuna masharti ya kutakiwa
kurejea gerezani lakini alisema Jaji Mkuu wa Zanzibar alisema ripoti na
uamuzi wa daktari utaheshimiwa kulingana na tatizo la kiafya
linalomkabili.
“Sijapewa
muda maalumu wa kurudi gerezani, kauli ya Jaji Mkuu, madaktari ndiyo
watakaoshauri kama nipumzike kwa muda gani kabla ya kurejeshwa rumande
na nina imani ripoti itakapowasilishwa watajadiliana,” aliongeza kusema
Sheikh Azzan.
No comments:
Post a Comment