Takribani watu 16 wamepoteza maisha leo jumanne kufuatia shambulizi
lililotekelezwa na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab katika kituo cha
polisi mjini Beledweyne nchini Somalia.Kwa mujibu wa mashuhuda ni kuwa
mwanachama mwanachama mmoja wa kundi hilo alijitoa mhanga kwa kujilipua
kwenye gari katika lango la kuingilia kituoni hapo kabla ya Makomandoo
wengine kuingia ndani na kuanza kuwafyatulia risasi watu waliokuwamo
ndani.Kwa upande wake Msemaji wa kundi hilo Abdulaziz Abu Musab ameliita
shambulizi hilo ni ushindi dhidi ya vikosi vya usalama vinavyoshiriki
oparesheni ya kuwatokomeza.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Jeshi nchini humo, Abdi Mohamed Ali waliouawa
ni wanajeshi na wengine ni raia wa kawaida. Aidha amethibitisha kuwa
polisi wamefanikiwa kuwaua watu wanne ambao ni wanachama wa Al Shabaab.
Naye kiongozi wa Al Shabaab, Kamanda Sheikh Mohamed Abu Suleiman
ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa shambulio hilo
liliwalenga maadui zao ambao ni wanajeshi wa Ethiopia, Somalia na
Djibout wanaoshirikiana na vikosi vya Umoja wa Afrika AMISOM.
Mwezi uliopita shambulio jingine lilisababisha vifo vya watu
takribani 15 katika mgahawa mmoja katibu na mpaka wa Ethiopia, Al
Shabaab pia walikiri kuhusika na tukio hilo lililowalenga wanajeshi wa
Ethiopia na wangine wa kikosi cha Umoja wa Afrika AMISOM.
Wanamgambo hao walitimuliwa kutoka katika ngome zao kubwa nchini
Somalia lakini bado wameendelea kuwa tishio kwa usalama wa nchi hiyo na
Afrika Mashariki.
Hivi karibuni Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC
liliidhinisha pendekezo la kuongeza wanajeshi zaidi ili kuzidisha nguvu
ya kupambana na wanamgambo hao.
Via kiswahili.rfi.fr
No comments:
Post a Comment