Dereva wa
pikipiki ya abiria maarufu kama bodaboda jina halijafahamika mpaka sasa
(kwani hawezi kuongea) amepata ajali mbaya na kuvunjika kabisa mguu
wake wa kulia mara baada ya kugongwa na roli la mchanga katika eneo la
daraja la Mkolani wilayani Nyamagana nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Kwa
mujibu wa Mwandishi wetu aliyeweza kuwahi kufika ktk eneo la tukio na
kutoa msaada wa gari kumfikisha dereva wa pikipiki hiyo aliyopata ajali
Hospitali ya Rufaa ya Bugando, annasema kuwa dereva huyo alikuwa
akitokea Mkolani kuelekea Buhongwa na Roli hilo lilikuwa likitokea
Buhongwa kuelekea Mkolani, imetokea wakati dereva wa roli 'akiovateki'
daladala iliyokuwa mbele yake ikibeba abilia, hivyo alipoipita tu
daladala hiyo akakutana uso kwa uso na bodaboda.
Baadhi ya
bodaboda na wasamalia wema wakimbeba majeruhi kumpeleka kwenye gari la
MSD Kanda ya Ziwa ili kumkimbiza hospitali ya Bugando.
Hivi ndivyo mguu ulivyo vunjika baada ya kupata ajali.
Sambamba na kuvunjika mguu pia dereva huyo amevunjika vidole vitatu vya mkono wake wa kulia. Na Mdodosoaji
No comments:
Post a Comment